Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi wamwacha Sheikh Ponda kwa dhamana
Habari Mchanganyiko

Polisi wamwacha Sheikh Ponda kwa dhamana

Sheikh Issa Ponda Issa, Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Tanzania akiwa mahakamani katika moja ya kesi zake
Spread the love

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, ameachwa na Jeshi la Polisi kwa dhamana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Ibrahim Mkondo ambaye ni Katibu wa Sheikh Ponda amesema, Sheikh Ponda ameachwa leo tarehe 20 Julai 2020, mchana.

“Sheikh ametoka leo, ameambiwa kesho saa 2 anatakiwa kuripoti polisi,” amesema Mkondo.

Sheikh Ponda alikamatwa tarehe 11 Julai 2020, alipokuwa ofisini kwake katika Msikiti wa Bungoni, jijini Dar es Salaam kwa madai ya kuandika waraka wenye uchochezi.

Kwenye waraka huo uliosomwa na Sheikh Ponda Issa Ponda, tarehe 9 Julai 2020 jijini Dar es Salaam, miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye waraka huo ni pamoja na kuitaka serikali kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu unakuwa huru na haki, pia umuhimu wa kuwa na Katiba Mpya.

“Kwa hakika maelezo yetu ya nini tunataka kwa taifa letu katika uchaguzi huu, yangekuwa na maana sana kama Taifa lingekuwa na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Tume Huru ya Uchaguzi, vinavyotokana na Wananchi wenyewe,” alisema Sheikh Ponda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!