October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kanye West aanza kampeni za urais Marekani

Kanye West

Spread the love

KANYE West, mwamauziki wa mtindo wa kufoka foka, ameanza safari ya kutaka kuwa rais wa Marekani kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Tayari amefanya mikutano katika miji ya Charleston na South Carolina. Hata hivyo, mikutao yake inaelezwa kutokuwa na msisimko kama mgombea urais. West (43) anawania urais kupitia chama chake cha Birthday Party.

Hata hivyo, mwanamuziki huyo amekumbana na kejeli kutoka kwa wakazi wa miji mbalimbali ya nchi hiyo, kwamba anachokifanya West ni kutaka umaarufu.

Katika mkutano wa Charleston, hakuonesha kuwa na maandalizi ya kufanya mkutano huo lakini wakati anaanza kampeni zake, kwenye ukurasa wake wa Twitter, ulionesha nyimbo za albamu anayotaka kutoa, jambo ambalo limeongeza maswali.

Akiwa amenyoa nywele sehemu ya nyuma ya kichwa chake, alizungumza na watu waliomzunguka bila kutumia kipaza sauti.

Mara kadhaa alikuwa akiwataka watu watulie pale alipoulizwa maswali ili asililize kutokana na kuwepo kwa msongamano wa watu, bila kuwepo kwa teknolojia yoyote ambayo ingerahisisha mawasiliano.

Moja ya sera zake ni kuhusu utoaji wa mimba, alimwaga chozi akisema mama yake nusura amtoe uhai akiwa tumboni mwake. Hata hivyo, amesema utoaji huo uendelee lakini sheria zifuatwe.

error: Content is protected !!