Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polepole: Mikutano kura za maoni iwe wazi, waandishi wa habari…
Habari za Siasa

Polepole: Mikutano kura za maoni iwe wazi, waandishi wa habari…

Spread the love

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humprey Polepole ameitaka mikutano ya majimbo na wilaya ya kura za maoni ya kupata wagombea udiwani, ubunge na uwakilishi ndani ya chama hicho iwe wazi kwa vyombo vya habari kushiriki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea)

Polepole  ametoa wito huo leo Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelekea shughuli ya kuwaopata wagombea udiwani, ubunge na uwakilishi ndani ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Amesema, uwazi aliouonyesha mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Pombe Magufuli katika mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM na mkutano mkuu iliyoanza tarehe 10 hadi 11 Julai 2020 jijini Dodoma unapaswa kuigwa katika mikutano ya kura za maoni.

Katika mikutano hiyo, hasa wa NEC ambao kwa mara ya kwanza ulirushwa moja kwa moja na vyombo vya habari ambao pamoja na mambo mengine, ulipiga kura za kumpanga mgombea urais wa Zanzibar na kumpendekeza Rais Magufuli kuwa mgombea urais wa Tanzania.

Vyombo vya habari vilishiriki mwanzo, mwisho ikiwemo uhesabuji wa kura ambapo Dk. Hussein Ali Mwinyi aliibuka mshindi kwa kupata kura 129 sawa na asilimia 78.65, Shamsi Vuai Nahodha kura 16 na Dk. Khalid Salum Muhamed akipata kura 19

Soma zaidi hapa

Ccm yapiga ‘stop’ michango holela za ubunge na udiwani

Polepole amesema, hilo linapaswa kuigwa na mikutano ya kura za maoni kwa wagombea kuruhusiwa wao wenyewe kushiriki kuhesabu kura zao na kama kamati za siasa, zitakuwa na uwezo wa kuarika vyombo vya habari kurusha moja kwa moja wafanye hivyo ili kuendeleza kile alichokiasisi Rais Magufuli.

Shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za udiwani, ubunge na uwakilishi unaanza kesho Jumanne tarehe 14 hadi 17 Julai 2020.

Soma zaidi hapa

Wahariri Tanzania wataka uwazi wa CCM uhamie NEC, Mahakama na Bunge

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!