Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yapiga ‘stop’ michango holela fomu za ubunge, udiwani
Habari za SiasaTangulizi

CCM yapiga ‘stop’ michango holela fomu za ubunge, udiwani

Humphrey Polepole, akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kimesema, mwanachama wa chama hicho anayetaka kuwania udiwani, ubunge au uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2020 asilazimishwe kutoa michango. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea)

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 13 Julai 2020 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu uchaguzi wa madiwani, ubunge na uwakirishi ndani ya chama hicho tawala.

Polepole ametoa kauli hiyo siku moja imebaki kabla ya shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa  fomu za kuwani udiwani, ubunge wa jimbo, uwakilishi, ubunge wa viti maalum kuanzia kesho Jumanne tarehe 14 hadi 17 Julai 2020.

 

Polepole amesema, CCM inazuia, “michango holela katika kipindi hiki cha uchaguzi. Kila kitu kinachofanyika lazima kifanyike kwa mujibu wa Katiba na kanuni zetu.”

“Michango yote, lazima ijadiliwe na ipitishwe na kamati za siasa za eneo husika. Michango ya aina yoyote ya mwanachama, inabaki kuwa michango ya hiari, ni marufuku mwana CCM kulazimishwa kuchanga,” amesema

Polepole amesema, “katu na kamwe aslani, michango isiwe kigezo cha kumnyima au kumpa fomu mwana CCM. Wagombea wapewe fomu sawa sawa na viwango vilivyoainisha.”

Amesema, nafasi ya udiwani ni Sh.10,000, ubunge na uwakilishi Sh.100,000, Ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Sh. 100,000 na nafasi ya Spika wa Baraza la Wawakilishi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sh.500,000.

“Kama ukimpa fomu, unamweleza chama kimepitisha harambee, sasa iwe hiari yake kuchangia au kutokuchangia, ndani ya vikao tutaona huyu amejitoa ndani ya chama huyu hajajitoa ndani ya chama lakini isitumike kama kigezo cha kumnyima fomu,” amesema Polepole

Polepole ametumia fursa kupiga marufuku wanachama wa chama hicho wanaotumia mitandao ya kijamii kujitangaza ‘kutia nia’ akisema ni kosa na watakaoendelea watachukuliwa hatua.

 

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!