Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NCCR-Mageuzi yamkana mgombea wake wa urais
Habari za Siasa

NCCR-Mageuzi yamkana mgombea wake wa urais

Spread the love

CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimekana kuutambua msimamo wa aliyekuwa Mgombea wake wa urais wa Tanzania, Yeremia Maganja wa kukubali matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

NCCR-Mageuzi kimesema, hakikubaliani na matokeo ya uchaguzi huo kwani ulikithiri ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi huo na kutaka uwepo wa meza ya majadiliano ili kuondoa sintofahamu iliyopo na kurejesha Taifa kwenye umoja.

“Uchaguzi ni mchakato, kanuni na miongozo ya uchaguzi vyote hivi vimekiukwa na vinapelekea matokeo kutokuwa halali ya kinachoitwa uchaguzi. Kwa sasa ni sawa na hakuna aliyeshinda wala aliyeshindwa,” amesema Edward Sembeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR Mageuzi.

Wakati NCCR-Mageuzi kikitoa msimamo huo leo Jumanne tarehe 3 Novemba 2020, Maganja alikuwa miongoni mwa wagombea urais wa vyama vingine waliohudhulia hafla ya kumpabidhi cheti cha ushindi, mgombea mwenzao kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli.

Hafla hiyo ilifanyikia Jumapili tarehe 1 Novemba 2020, Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) zilizopo Njedegwa jijini Dodoma ambapo Dk. Magufuli na mgombea wake mwenza, Samia Suluhu Hassan walikabidhiwa vyeti hivyo na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage.

Edward Sembeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma wa NCCR Mageuzi

MwanaHALISI Online limetaka kujua kutoka NCCR-Mageuzi juu ya mgombea wake wa urais Maganja kuhudhulia hafla hiyo huku kikiwa hakitambua matokeo yanayotokana na matoke hayo, Simbeye amesema msimamo huo wa Maganja kwenda kuhudhulia hafla hiyo ni wake binafsi wale chama hakikuwa kikifahamu.

“Mgombea urais wa chama chetu alikwenda Dodoma kama mtu binafsi, hakutumwa na chama na hakuambiwa na chama akafanye hivyo. Hatuwezi kuingilia uhuru wake wa kusafiri au kwenda anakotaka,” amesema Simbeye.

Simbeye amesema, hatua hiyo ilikuwa matamanio yake binafsi Maganja hasa ikizingatiwa chama kilikuwa hakijatoa tamko lolote kuhusu uchaguzi huo na endapo, baada ya msimamo huo kutolewa leo, akiendelea chama hakitasita kuchukua hatua.

“Angefanya baada ya tamko hili kwa maana kesho angeshiriki, tungezungumza mambo mengine kwa kuwa amekwenda kabla ya tamko la chama bado sisi tunaona hayo ilikuwa matamanio yake binafsi na ilikuwa ni uhuru wake ila hakuagizwa na chama chetu na hakuwasiliana na kiongozi wa chama,” amesema Simbeye.

Yeremia Maganja wa NCCR-Mageuzi kuwa mgombea urais wa Tanzania

Kutokana na mkanganyiko huo, Simbeye amesema NCCR-Mageuzi kitafanya kikao na Maganja kwa ajili ya kujadili msimamo wake huo.

“Kwa sasa baada ya kutoa msimamo wa chama, vikao vingine vitaendelea na mgombea urais atashirikishwa, mambo mengine yatazungumza ndani ya vikao,” amesema Simbeye.

Alipoulizwa kama NCCR-Mageuzi itamchukulia hatua gani Maganja iwapo ataendelea kushiriki iwapo kuhudhulia sherehe za kuapishwa Rais mteule Magufuli Alhamisi tarehe 5 Novemba 2020 Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Simbeye amesema, kwa sasa hawezi zungumzia suala hilo kwani halijatokea.

“Adhabu ya mtu hutokana na tukio alilolifanya, kwa hiyo hatuwezi kutabiri nini kitatokea mpaka mazingira yatavyo amua. Ikiwa litatokea siwezi kusema adhabu gani ama kitu gani tutafanya itoshe kusema tu  tutavuka mto, tukifika mtoni,” amesema Simbeye

Baadhi ya wagombea hao waliohudhuria akiwemo Maganja ni; Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini), Queen Sendiga (ADC), Muttamwega Mgaya (SAU), John Shibuda (Ade Tadea), Leopard Mahona (NRA), Twalib Kadege (UPDP), Seif Maalim Seif (AAFP), Philip Fumbo (DP) na Khalifan Mazurui wa UMD.

Wagombea ambao hawakuhudhulia; Bernard Membe (ACT-Wazalendo), Hashim Rungwe (Chaumma), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na Tundu Lissu wa Chadema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!