Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai, Dk. Tulia wajitosa Uspika
Habari za Siasa

Ndugai, Dk. Tulia wajitosa Uspika

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania
Spread the love

JOB Yustino Ndugai, Mbunge mteule wa Kongwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amejitosa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea Uspika wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ndugai ambaye ni Spika wa Bunge la 11 lililomaliza muda wake amechukua na kurejesha fomu hiyo Ofisi za Makamo Makuu CCM, Dodoma leo Jumanne tarehe 3 Novemba 2020.

Wakati Ndugai akitaka kutetea nafasi hiyo, Dk. Tulia Ackson, mbunge mteule wa Mbeya Mjini kupitia CCM naye amechukua fomu ili atetee nafasi ya Naibu Spika wa Bunge.

Spika Ndugai akizungumza na waandishi baada ya kuchukua fomu amesema, amepewa fomu ambazo amezijaza na kuzirejesha kwa mujibu wa utaratibu wa chama hicho tawala nchini Tanzania.

“Nafasi ya Uspika, inajazwa kwa wanaopendekezwa na vyama vya siasa na nia yangu na kama chama changu kitanikubalia kuwa Spika wa Bunge la 12. Kipaumbele chetu na fikira zetu, kwa sasa niombe Watanzania chama changu kiweze kuniruhusu ili niwe Spika,” amesema Ndugai

Kwa upande wake, Dk. Tulia amesema, hizo ni nafasi za utumishi “niko tayari kutumika na miaka mitano nilifanya katika nafasi hiyo. Shauku yangu ni kuona wabunge wakiwakilisha wananchi waliowachagua kwa kuwaleta bungeni kwani mule ndani kuna vyama vingi.”

Dk Tulia amesema “katika utumishi huu ni kuona wabunge wakifanya vizuri kwa kuwawakilishi na kuikumbusha Serikali kile wananchi wao wanakitaka na wameahidiwa.”

Dk. Tulia Ackson akipokea fomu ya kuwania nafasi ya Unaibu Spika katika Bunge la 12 la Tanzania

“Tutarajie uwakilishi mzuri, mimi huwa nawaza mambo mazuri na wananchi wamechagua wawakilishi ambao wameona wao wanafaa na mimi kama mwenyezi Mungu atanipa fursa ya kuongoza mambo yatakwenda vizuri,” amesema

Dk. Tulia amesema, ameamua kuchukua nafasi ya naibu spika kwani amejipima na kuona hiyo inamfaa hasa ikizingatiwa atakuwa na majukumu mengine ya uwakilishi wa wananchi wa Mbeya Mjini hivyo atahitaji muda zaidi ya kuwatumikia.

Jana Jumatatu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alitoa taarifa kwa umma akiwataka wanachama wa chama hicho wanaotaka kuwania Uspika, Naibu Spika, Meya wa halmashauri ya jiji, manispaa na mwenyekiti wa halmashauri za wilaya kujitosa kuwania nafasi hizo.

Fomu za kuwania nafasi hizo zilikuwa zinatolewa kuanzia jana na kuhitimishwa leo Jumanne saa 10:00 jioni.

Polepole alisema, kesho tarehe 4 Novemba 2020 Kamati za Siasa za Wilaya za CCM zitajadili maombi ya waliojitokeza na kutoa mapendekezo tarehe 5 Novemba 2020 kamati za siasa za mikoa zikutane kujadili kisha zitoe mapendekezo.

Alisema, mapendekezo ya kamati za siasa za wilaya na mikoa yawe yamefika ofisini kwa katibu mkuu wa CCM jijini Dodoma si zaidi ya saa 10:00 jioni tarehe 6 Novemba 2020

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!