Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Mwanafunzi aliyepewa ujauzito, achonga dili na aliyempachika
ElimuHabari Mchanganyiko

Mwanafunzi aliyepewa ujauzito, achonga dili na aliyempachika

Mwanafunzi mjamzito
Spread the love

JASON Rwekaza, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore, Kigoma anayetuhumiwa kumpa ujauzito mwanafunzi wake (jina linahifadhiwa), amekamatwa tena. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mwalimu huyo awali aliachwa huru na Jeshi la Polisi, lakini amekamatwa tena kwa tuhuma za ‘kuchonga dili’ na mwanafunzi huo la kuharibu ushahidi jambo lililosababisha kuachwa huru.

Jeshi hilo limeeleza kwamba Rwekeza alikula njama na mwanafunzi wake, ili aharibu ushahidi hivyo kufutiwa mashtaka ya ubakaji yaliyokuwa yakimkabili.

Leo tarehe 18 Septemba 2019, Martin Otieno ambaye ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kigoma amesema, Rwekaza anashikiliwa na polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi, hadi pale shauri dhidi yake litakapofikishwa mahakamani, kisha mahakama hiyo itaamua kama atapewa dhamana au la.

Kamanda Otieno ameeleza, uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi, umebaini kwamba Rwekaza anahusika kwenye njama za mwanafunzi kubadilisha maelezo aliyotoa awali polisi na yale aliyotoa mahakamani katika kesi ya ubakaji, na kupelekea kesi hiyo kufutwa.

Tarehe 16 Septemba 2019, Rwekaza aliachwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma baada ya mwanafunzi huyo kuvuruga ushahidi, kwa kuieleza mahakama hiyo kwamba, hamfahamu mtu aliyempa ujauzito na kwamba,  ana umri wa miaka 19.

Maelezo hayo yalikuwa tofauti na yale aliyotoa awali mwanafunzi huyo alipohojiwa polisi, ambapo alisema ana umri wa miaka 16. Pia, Sakina Kazili, mama mzazi wa mwanafunzi huyo hadi sasa anashikilia maelezo yake kwamba mtoto wake, ana umri wa miaka 16.

 Kufuatia sintofahamu hiyo, Kamanda Otieno amesema, Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi wa sakata hilo kwa upande wa wanafunzi huyo, kisha kufungua jalada dhidi ya mwanafunzi huyo kwa tuhuma za kutoa ushahidi wa uongo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!