MFANYABIASHARA maarufu nchini na mwekezaji katika Klabu ya Simba, Mohamed Dewj ‘Mo’ ameanzisha mjadala mtandaoni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Tarehe 17 Septemba 2019, Mo aliweka ujumbe wake kwenye ukurasa wake wa twitter akisema ‘kuna maisha ya mtandaoni na maisha halisi.’
Kauli hiyo imepokewa kwa mtazamo tofauti ikizingatiwa kwamba, kutekwa kwake kulisababisha kuanzishwa kwa kampeni mtandaoni iliyokwenda kwa jina la ‘BringBackMo’.
“@moodewji Zamani nilizoea kusikia mipasho na kejeli kwa Mzee Yusuf siku hizi mipasho imeamia kwa viongozi wa siasa hadi soccer napita tu:” mchangiaji wa kwanza aliandika huku wengine wakifuata
Hata hivyo, baada ya ujumbe wake huo kwenye ukurasa wake wa twitter, Maria Sarungi ambaye ni mwanaharakati, ndiye aliyemchokonoa zaidi pale alipoandika ‘#BringBackMo ilikuwa maisha ya mtandaoni au maisha halisi?’
Swali hilo liliwavuta wachangia wengi ambao baadhi yao walionekana kuwa na tafsiri zilizotofautiana, wengi wakionesha kutasiri ujumbe wa Mo kwa mtazamo hasi.
Mmoja wa wachangiaji wa twitter ya Sarungi alianza kwa kuhoji ‘Leo ndio tumekuwa “wa mitandaoni” lkn kumbuka kelele zetu ndio zilisaidia wewe kuachiwa na watekaji wako. Unless utuambie ule ulikuwa mchezo wa kutafuta umaarufu @moodewji.’
Kutokana na jumbe mbalimbali zilizokuwa zikitolewa mtandaoni, Mo alirejea na kuomba radhi “Nisamehe sana dada yangu. Naona umeichukulia tweet yangu out of context. Narudia kuwashukuru wote ambao mliniombea ne kunisemea.”
Leave a comment