December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

M/Kiti BAVICHA afunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

Spread the love

AYUBU Sikagonamo, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA), Mkoa wa Songwe amefutiwa kesi ya kukutwa na silaha, na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BAVICHA kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Sikagonamo amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Momba leo tarehe 18 Septemba 2019 na kubadilishiwa shitaka.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Sikagonamo alifikishwa mahakamani hapo na kufutiwa kesi ya awali ya kukutwa na silaha, kisha kukamatwa tena na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi Namba 10 ya mwaka 2019.

Taarifa hiyo ya BAVICHA inaeleza, kesi hiyo itaanza kusikilizwa tarehe 2 Oktoba 2019.

Sikagonamo alikamatwa na Jeshi la Polisi Julai mwaka huu, akituhumiwa kukutwa na silaha nyumbani kwake eneo la Mwaka katika Kata ya Chipaka, Tunduma mkoani Songwe.

error: Content is protected !!