October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jengo Old Tanga Sekondari lateketea

Spread the love

JENGO moja la Shule ya Sekondari ya Old Tanga, iliyoko jijini Tanga limeteketea kwa moto mchana wa leo tarehe 18 Septemba 2019. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Tukio hilo limethibitishwa na Edward Bukombe, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Tanga, aliyesema kwamba moto huo ulizuka majira ya saa 6.00 mchana.

Kamanda Bukombe amesema, hadi sasa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Hata hivyo, amesema moto huo haujaleta madhara.

“Kuna jengo moja ambalo ni ukumbi, ni jengo la zamani tangu enzi ya mkoloni limeungua lote kwa moto. Bado hatujajua chanzo chake. Lakini haujaleta madhara yoyote kwa binadamu,” amesema Kamanda Bukombe.

error: Content is protected !!