Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mengi awapa ‘dili’ vijana katika hali ngumu
Habari Mchanganyiko

Mengi awapa ‘dili’ vijana katika hali ngumu

Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF), Reginald Mengi
Spread the love

MWENYEKITI wa Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) Reginald Mengi, amewaomba vijana kuchangamkia fursa za kibiashara zinazojitokeza wasipotoshwe na msemo wa hali ngumu, wakati huo kuna wageni wanakuja kutoka nje ya nchi wanapata kazi za kufanya. Anaripoti Angel Willium … (endelea).

Akizungumaza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mtandao wa Mitaji ya Ubia, Mengi amesema vijana wengi wamekuwa wanalalamika hali ngumu huku kuna watu wanafanikiwa katika kipindi hiki hivyo wanatakiwa kuwa na macho ya kibiashara.

Mengi amesema vijana wawe tayari kujifunza na kupata mawazo mapya huo ndiyo mwanzo wa mafanikio na kuheshimu sheria za nchi na kuzifuata katika biashara kama kulipa kodi nakutoficha kazi wanazofanya katika maeneo yao.

“Vijana wanatakiwa kujiamini katika biashara na kusema wanaweza, pia wanatakiwa kuaminia na kueshimiana wakati wa kufanya kazi,” amesema Mengi.

Aidha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Faustin Kamuzora amesema, mtandao wa Mitaji ya Ubia utasaidia wenye makapuni kuongoza watu iliwaweze kukuwa katika kufanya kazi, watanzania wengi wamezoea kupata pesa za biashara katika familia au kukopa lakini hii itawasaidi kujua vitu vingi.

Kamazora amesema kampuni ikiwa kubwa inaweza kuvutia wale wenye mitaji kuja kujiunga nao hata wafanyabiashara wa nje wanaweza kuingia na kuwekeza hadi pale biashara inapokuwa, suala hili huko nje linatumika sana katika kufanikisha makapuni yaingie ubia.

Pia Kamuzora amesema, Watanzania watakaokuwa tayari wanakaribishwa kujiunga na mtandao huo kwani ni njia nyepesi ya kupata mtaji mkubwa wa kibiashara na watapata elimu kuhusu uwekezaji.

Mtandao wa Mitaji ya Ubia itawasaidia wenye makampuni kufanya biashara na watu wa nje ya nchi hivyo wataweza kuongeza ufanisi wa kufanya kazi na kuendesha kampuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!