March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Afya ya Mbowe yazidi kuimarika

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

AFYA ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe inazidi kuimalika baada ya kufikishwa kwenye hospitali na Rufaa ya KCMC jana jioni akiwa huku afya yake ikiwa sio shwari. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa Msemaji wa hospitali hiyo, Gabriel Chisseo ameeeza kuwa Kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni alifikishwa hospitali hapo akiwa na maumivu makali ya kichwa. 

Chisseo ameeleza kuwa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali zinaonesha mbunge huyo ana uchovu.

“Taarifa zinaonyesha alikuwa na maumivu ya kichwa. Taarifa za kitabibu zinaonyesha ni uchovu,” ameeleza Chisseo.

Chasseo ameleeza kuwa Mbowe amepumzishwa kwenye hosiptali hiyo akiendelea kupatiwa matibabu na kwamba anaendelea vizuri. “Wataalamu wanaendelea kumhudumia kwa ukaribu baadaye atafanyiwa vipimo vingine.”

error: Content is protected !!