Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mdee, Bulaya kushtakiwa kwa vurugu gerezani
Habari za Siasa

Mdee, Bulaya kushtakiwa kwa vurugu gerezani

Halima Mdee
Spread the love

HALIMA Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na Esther Bulaya, Mbunge wa Bunda mjini, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kufanya fujo gerezani Segerea, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam …  (endelea).

Watafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam pamoja na wafuasi 25 wa chama hicho ambao walihusishwa na vurugu zilizotokea tarehe 13 Machi 2020 wakati walipokwenda kumtoa mwenyekiti Freeman Mbowe.

Mbowe alitarajiwa kutoka gerezani ambako alipelekwa sambamba na viongozi wenzake wanane mara baada ya kuhukumiwa tarehe 10 Machi 2020 kulipa faini ya jumla ya Sh. 350 milioni au kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi mitano gerezani kila mmoja.

Walikuwa wametiwa hatiani kwa makosa ya uchochezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba aliyesema ameona huruma kutoa adhabu hiyo kwa kuwa baadhi yao walishakaa gerezani wakati kesi ikiendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 15 Machi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Lazaro Mambosasa amesema hatua hiyo inafuatia kukamilika kwa upelelezi wa makosa yao.

“Baada ya watuhumiwa kukamatwa askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la Magereza waliwapeleka kituo cha Polisi cha Stakishari kwa mahojiano ambayo yaliwathibitishia kuhusika kwao na fujo kwa kutaka kuingia gerezani kwa nguvu,” amesema.

“(Ofisi yangu) tulipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa Gereza la Mahabusu Segerea kuwapo kwa kundi la wafuasi wa Chadema likiongozwa na wabunge wawili Mdee na Bulaya pamoja na Meya wa Ubungo Boniface Jacob lilokusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo,” amesema SACP Mambosasa.

SACP Mambosasa huku akionya dhidi ya vitendo vya vurugu kwenye maeneo nyeti kama gerezani, amesema si mtindo mzuri kwa mtu yeyote au kikundi chochote cha siasa au dini kuchezea maeneo hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!