Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko MCT ‘jino kwa jino’ na Serikali ya Awamu ya Tano
Habari MchanganyikoTangulizi

MCT ‘jino kwa jino’ na Serikali ya Awamu ya Tano

Kajubi Mukajanga, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT). Picha ndogo Alexander Mnyeti aliyewahi kumweka mahabusu mwandishi
Spread the love

BARAZA la Habari Tanzania (MCT), limepaza sauti na kusema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita hofu kwa waandishi wa habari na tasnia nzima imeongezeka na kusababisha wanataalum hao kutofanya kazi kwa uhuru na kwa weledi, anaandika Faki Sosi.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kuhusu siku ya Kimataifa ya Kupinga Jinai Dhidi ya Wanahabari ambayo inaadhimishwa duniani kote.

MCT imesema katika kipindi hicho kumekuwapo na matumizi mabaya ya madaraka, upindishwaji wa sheria, unyanyasaji na hata matamsihi ya vitishio kutoka kwa viongozi wa serikali dhidi ya wanahabari na vyombo vyao.

Amesema katika kipindi hicho wanahabari mbalimbali wamenyanyaswa pamoja na magazeti sita kufungiwa na serikali kufanya uzalishaji kwa madai kwamba yaliandika habari za uchochezi ambazo hazitakiwa na watawala.

Mukajanga amesema kuanzia sasa MCT itaanza kuwafikisha mahakamani watu wote wanawazuia, kuwanyanyasa na kuwapiga wanahabari wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

Amesema lengo la MCT na washirika wake ni kuhakikisha inamshtaki mtu mmoja mmoja iliawajibke kwa matumizi mabaya ya madaraka au kwa unyanyasaji.

Ameongeza kuwa MCT inaamini mahakamani ndiyo mahala ambapo haki inatendeka na kwamba linahimiza vyombo vya habari na wananchi kuunga mkono juhudi zake na wadau wengine wa habari kushinikiza ili zifutwe sheria kandamizi zinazofifisha uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari na haki ya kupata taarifa.

Amewakumbusha viongozi wa vyombo vya habari hususani wamiliki, watendaji wakuu na wahariri kuhakikisha wanawalinda waandishi na kuzingatia usalama wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!