March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

EU yamwaga fedha kwa ajili ya umeme vijijini

Fundi umeme wa Tanesco akiunganisha umeme wa REA katika moja ya nyumba zilizopo kijijini

Spread the love

UMOJA wa Ulaya (EU), umetoa msaada wa Euro Milioni 50 ambazo ni sawa na takribani Sh. bilioni 130 kwa ajili ya miradi ya usambazaji wa umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), anaandika Richard Makore.

Makubaliano ya msaada huo yamesainiwa jijini Dar es Salaam leo kati ya EU ukiwakilishwa na Kamishna wa Maendeleo wa Umoja huo, Neven Mimica na Serikaliya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango ikiwakilishwa na Katibu Mkuu wake, Dotto James.

Katika mkutano huo, Wizara ya Nishati iliwakilishwa na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Nishati Jadidifu Ishengoma.

Akizungumza kabla ya kusaini makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James alisema kuwa kiasi hicho cha fedha ni sehemu ya awali ya kiasi cha Euro milioni 180 zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha Sekta ya Nishati na kufafanua kuwa fedha hizo zitatolewa katika Awamu mbalimbali.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo, Euro milioni 90 zitatumika kwa ajili ya mpango wa kusambaza umeme vijijini kupitia REA na nyingine Euro milioni 90 zitatumika kwa ajili ya kuboresha Sekta ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na REA.

Aliendelea kusema kuwa msaada huo usio na masharti ni moja ya mikakati ya EU ni kuunga mkono juhudi za Serikaliya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli katika usambazaji wa Umeme Vijijini.

Katika hatua nyingine, James aliushukuru EU kwa msaada huo na kusisitiza kuwa Serikaliitautumia msaada huo katika kuhakikisha kuwa vijiji vyote Tanzania vinapata Umeme ifikapo mwaka 2020.

Awali akielezea mafanikio ya REA, James alisema wakati REA inaanzishwa mwaka 2008 asilimia mbili tu ya vijiji vyote vilikuwa vinapata Umeme lakini hadi kufikia Desemba, 2016 ni asilimia 49.3 wananchi waishio vijijini wanapata Umeme.

Amefafanua kuwa mwaka 2008 asilimia 10 ya wananchi kitaifa walikuwa wanapata umeme (overall electricity access level) lakini hadi kufikia Desemba, 2016 ni asilimia 67.5 wanapata Umeme wa uhakika.

“Mafanikio haya ni makubwa na ninaamini kupitia msaada huu na ongezeko la kasi ya usambazaji wa Umeme vijijini, ifikapo mwaka 2020 vijiji vyote nchini Tanzania vitakuwa na Umeme wa uhakika na kupelekea kwenda kwenye uchumi wa Viwanda,” alisema James.

Wakati huo huo akizungumza kabla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Kamishna wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya (EU), Neven Mimica alisema kuwa Umoja huo unatambua juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati katika usambazaji wa Umeme vijijini hivyo wapo tayari kuisaidia Serikaliili iweze kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa yenye lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Ameongeza kuwa umeme ni muhimu husan katika maeneo ya vijijini kwa kuwa inachangia uboreshaji wa huduma za jamii kama Shule, Vituo vya Afya, Hospitali, Viwanda vidogo vidogo na Kilimo.

Amesema kuwa kupatikanaji kwa nishati hiyo vijijini kutsaidia kuongeza ajira kwa wananchi kwa kuwa wataweza kujiajiri kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao.

error: Content is protected !!