Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mchanga wa dhahabu kumng’oa mwingine?
Habari MchanganyikoTangulizi

Mchanga wa dhahabu kumng’oa mwingine?

John Magufuli, Rais wa Tanzania akipokea ripoti kutoka kwa Profesa Abdulmalik Mruma Mwenyekiti wa Kamati ya kwanza ya Wataalam wa Jiolojia iliyoiundwa kwa ajili ya kuchunguza kiwango na aina ya madini yaliyopo kwenye mchanga wa madini (Makinikia)
Spread the love

RAIS John Magufuli anatarajia kupokea ripoti ya pili kuhusu usafirishaji wa mchanga wa dhahabau (maknikia) Jumatatu ya tarehe 12 Juni mwaka huu, ikiwa ni wiki tatu tu tangu apokee ripoti ya kwanza iliyosababisha kung’olewa madarakani kwa Profesa Sospeter Muhongo, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, anaandika Hamis Mguta.

Kamati ya kwanza iliyongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma illiundwa wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi, lakini kamati ya pili iliyo chini ya Prof. Nehemiah Eliachim Osoro na ambayo itawasilisha ripoti yake Jumatatu imesheheni wachumi na wanasheria tu.

Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, amesema tukio hilo litarushwa hewani moja kwa moja kupitia redio, televisheni, mitandao ya kijamii na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz kuanzia saa 3:30 asubuhi.

Rais Magufuli alipokea ripoti ya kamati ya kwanza yenye wajumbe wanane Mei 24, mwaka huu iliyochunguza viwango vya madini yaliyomo kwenye mchanga wa madini uliomo ndani ya makontena yaliyozuiliwa na Serikali kusafirishwa nje ya nchi.

Kamati hiyo iliteuliwa na Rais Machi 29, mwaka huu. Huku Kamati ya wanasheria na wachumi ikiteuliwa Aprili 10 mwaka huu.

Baada ya kuipokea ripoti hiyo, Rais Magufuli aliytengua uteuzi wa Prof. Muhongo huku akiahidi kuchukua hatua zaidi baada ya kupokea ripoti ya pili.

Sambamba na uamuzi huo lakini pia Rais aliivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kumsimamisha kazi mkurugenzi mtendaji wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!