Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Regina Lowassa awapa mbinu BAWACHA kuing’oa CCM
Habari za Siasa

Regina Lowassa awapa mbinu BAWACHA kuing’oa CCM

Regina Lowassa, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
Spread the love

BARAZA la wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) wametakiwa kuungana na kuweka mipango mikakati ya nguvu ili kuhakikisha wanaiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mama Regina Lowassa alipokuwa akizungumza na wanawake wa baraza hilo katika mkutano wao wa kikao cha ndani na kikao cha kazi kilichofanyika mjini Dodoma.

Amesema juhudi za akina mama wa Chadema zilizofanyika katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 zilikuwa na nguvu kubwa hivyo kuna kila sababu ya kuongeza nguvu zaidi ili kuhakikisha akina mama wanagombea nafasi mbalimbali kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa.

“Kwa sasa akina mama wenzangu kinachotakiwa ni kushikamana na kuwa na mikakati ya pamoja ili kuhakikisha mapambano ya kuing’oa CCM madarakani yanafanikiwa.

“Hakuna sababu ya kugombana wala kutofautiana ,wala kutegeana katika kufanya kazi, umefika wakati sasa wa kuanza nikakati ya pamoja katika kujenga chama,kujengeana uwezo pamoja na kutokuwa waoga katika kufanya maamuzi.

“Ni ukweli usiopingika katika uchaguzi wa mwaka 2015 CCM ilikuwa na wakati mgumu sana kwani akima mama mlionesha ujasiri mkubwa na mlifanya kazi nzuri na matokeo yake yalionekana,sasa uchaguzi umekwisha ni wakati wa kujipanga na kusonga mbele zaidi ili kuhakikisha CCM inaondoka madarakani ili kuwapa unafuu watanzania ambao wameteseka kwa muda mrefu sasa kutoka  na na chama hicho kuwa na mfumo kandamizi” amesema Mama Lowassa.

Naye Halima Mdee, Mwenyekiti wa BAWACHA akifungua kikao cha kazi cha baraza hilo amewataka akina mama kuhakikisha wanafanya kazi kwa ujasiri na kuhakikisha wanapata nafasi mbalimbali katika ngazi za maamuzi.

Mdee ametolea mfano wa mkutano wa baraza kuu la Chadema Taifa na kueleza kuwa katika baraza hilo watoa maamuzi wengi walikuwa wanaume jambo ambalo linaonesha wazi kuwa akina mama wengi hawajitokezi kugombea nafasi mbalimbali za kimaamuzi.

Kutokana na hali hiyo sasa napenda kuwahamasisha wabunge wote wa Viti Maalum, kuhakikisha wanatafuta majimbo na kutafuta nafasi mbalimbali za maamuzi badala ya kuwa na hofu na kujiona kana kwamba zipo nafasi mbalimbali ambazo zinafaa kugombewa na na wanaume na siyo wanawake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!