Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Mkenda: Wanasiasa msitupelekeshe
Habari za Siasa

Prof. Mkenda: Wanasiasa msitupelekeshe

Charles Mwijage, Waziri wa Viwanda, Biashara
Spread the love

PROFESA Adrof Mkenda, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, amewataka wanasiasa hapa nchini kuacha kuingilia masuala ya kitaalam yanayofonywa kwa kuzingatia utashi wa kitaaluma zaidi, anaandika Dany Tibason.

Pia amewaasa watumishi wa serikali kutokuwa tayari kufuata matakwa ya wanasioasa na badala yake wazingatie maadili na misingi ya kitaaluma katika majukumu yao.

Prof. Mkenda ameyasema hayo leo wakati akifungua semina ya wakurugenzi wa mipango na sera kutoka wizara mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hazina mjini Dodoma.

“Katika kufanya kazi za kutengeneza mipango na sera mbalimbali za kulinda ubora wa mlaji pamoja na usambazaji wa bidhaa, ni lazima tujiepushe na matakwa ya wanasiasa ambayo yamekuwa yakiingilia kazi za wataalam,” amesema.

Prof. Mkenda amesema ili kuimarisha ubora wa bidhaa nchini lazima mamlaka husika zinatakiwa kufanya ukaguzi wa bidhaa huku wakitoa elimu kwa jamii badala ya kutumia mabavu na mashambulio kwa watu ambao wanatoa huduma mbalimbali.

Amesisitiza kuwa, katika nchi ya Tanzania kuna sheria ya kufanya biashara huria lakini hairuhusu kuwa na biashara holela ili kulinda afya za walaji.

“Ili uweze kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa uaminifu ni lazima ujipambanue na kujiondoa katika viashiria vya rushwa. Kupenyeza rushwa kunaweza ni chanzo kikubwa cha kuzagaa kwa bidhaa bandia mitaani.

“Tujiulize wale askari walioruhusu gari lililosababisha vifo vya watoto 32 walimu 2 na dereva mmoja wa Shule ya msingi ya Lucky Vincent ya Arusha hawakuona kama watoto wamezidi katika gari hiyo na walikuwa wamevunja sharia? uzembe unaweza kuligharimu Taifa,” amesema Prof. Mkenda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!