January 16, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge upinzani akimbilia CCM

Spread the love

REHEMA Migira, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amekimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora…(endelea).

Akitangaza kwenye sherehe ndogo iliyofanywa na chama hicho Tabora leo tarehe 15 Juni 2020, Rehema amesema, amejiunga na chama hicho baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Taifa.

“Nikiwa na akili zangu timamu na kwa utashi wangu mimi mwenyewe, nimeamua kwa ridhaa yangu mimi mwenyewe bila kushikiwa mtutu wa bunduki kurudi chama cha mapinduzi,” amesema huku akipigiwa vigelegele na kuongeza:

“…maamuzi haya sikuyafanya eti kwa sababu napenda rangi za kijani, kuna sababu ambazo zimepelekea mimi leo niamue kurudi chama cha mapinduzi, CCM imekuwa ni ya wazalendo.”

Amesema, sera za CCM zinatekelezwa kupitia Rais Magufuli kwa kushirikiana na wasaidizi wake. “Vitendo hivyo vimesababisa hata sisi wapinzani tushawishike,” amesema.

error: Content is protected !!