Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mauaji ya watoto; IGP Sirro anasa waganga wa kienyeji 65
Habari Mchanganyiko

Mauaji ya watoto; IGP Sirro anasa waganga wa kienyeji 65

IGP Simon Sirro
Spread the love

JESHI la Polisi limekamata maganga 65 katika Mkoa wa Simiyu na Njombe kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji ya watoto yaliyotokea Januari 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Waganga 20 wamekamatwa katika Mkoa wa Njombe huku 45 wakikamatwa kutoka Mkoa wa Simiyu kutokana na operesheni ya kusaka wahusika wa maujai hayo yaliyotikisa.

“Tumekamata amabao tunawatilia shaka katika operesheni inayoendelea ya kuwasaka wahalifu hao,” ameeleza IGP Simon Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

 IGP Sirro alitangaza idadi hiyo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu upelelezi wa matukio ya mauji ya watoto yaliyotokea katika Mkoa wa Njombe na Simiyu.

“Kuna waganga ambao si wahalifu, lakini kuna wale waganga ambao ni wahalifu. Hao tunadili nao moja kwa moja na tayari tumeshakamata waganga 45 mkoani  Simiyu na waganga 20 mkoani Njombe,” alisema.

 Sababu za kuwapo kwa matukio ya mauaji ni ramli chonganishi, ugomvi wa familia na wivu wa mapenzi.

“Zipo sababu nyingi zinazofanya kuwapo kwa matukio haya, lakini kubwa ni ramli chonganishi kwa maana hiyo operesheni zinaendelea kwa kila mganga, lazima wapekuliwe wakaguliwe na wale watakaoonekana ni wahalifu na wanachofanya ni uvunjifu wa sheria, sheria itachukua mkondo wake,” alisema IGP Sirro.

IGP Sirro pia alisema, wamezielekeza halmashauri zifanye usajili wa waganga wa kienyeji na viongozi wa dini na siasa ili wasaidie kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matukio hayo.

Alisema, ipo mipango mikakati ambayo imewekwa na jeshi hilo kuhakikisha wanamaliza matukio hayo yaliyojitokeza nchini siku za hivi karibuni.

“Wanaofanya matukio hayo wasifikiri hawatabainika ipo siku yao tu na tukiwakamata tutawachukulia hatua stahiki,” alisema IGP Sirro.

Pia, alisema licha ya matukio ya uhalifu wa kutumia silaha na biashara za dawa za kulevya kupungua nchini, matukio ya ubakaji yamekithiri.

Alisema, Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana nayo kwa kuanza kutoa elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu ili kuepuka tatizo hilo.

IGP Sirro alisema, “Sababu kubwa ya kukithiri kwa matukio haya ni mmomonyoko wa maadili. Licha ya adhabu kali zinazotolewa kwa watuhumiwa wa matukio haya.

“Jeshi la polisi limejipanga kutoa elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu, kubandika na matangazo yanayoelezea madhara ya matukio ya ubakaji,” alisema.

Aliwataka wanasiasa na  viongozi wa dini waanze kutoa elimu katika jamii ili wajue jinsi ya kukabiliana na tatizo hilo ambalo linakatisha ndoto za watoto wa kike.

Mwezi Januari, mwaka huu, mkoani Njombe kuliripotiwa matukio ya utekaji na mauaji dhidi ya watoto,  wanaotekeleza ukatili huo hukunyofoa baadhi ya viungo kwenye miili ya watoto wanaowaua ambayo inaashiria kuwa ni mambo ya kishirikina.

Tayari watu kadhaa wameripotiwa fikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka  huku wengine wakiendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na matukio hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!