Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Marufuku kulima mahindi ndani ya Jiji la Dodoma
Habari Mchanganyiko

Marufuku kulima mahindi ndani ya Jiji la Dodoma

Mahindi yakiwa shambani
Spread the love

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amepiga marufuku kulima kilimo cha mazao ya mahindi, mtama na uwele katika kata 20 ambazo zipo ndani ya Jiji. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea). 

Ametoa kauli hiyo jana alipokuwa akiwasilisha mada mbalimbali katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Dodoma kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo  Vijijini jijini hapa.

Kunambi alisema kuwa kati 20 ambazo zipo ndani ya Jiji la Dodoma hazitakiwi kuendesha kilimo cha mazao marefu na badala yake mazao ambayo yanatakiwa kulimwa ni mazao ambayo ni ya bustani ya mboga mboga.

“Kutokana na hadhi ya Jiji ni marufuku kuendesha kilimo cha mahindi, mtama na uwele katika kata 20 zilizopo ndani ya jiji ila kinaweza kufanyika kilimo cha bustani na mbogamboga na jambo kubwa zaidi ni kuhakikisha uasafi ndani ya Jiji ukizingatiwa zaidi,” alisema Kunambi.

Mbali na mkurugenzi kutangaza kata hizo kutolima mazao marefu ndani ya kata hizo mmoja wa madiwani kutoka kata ya Majengo Mayaoyao Msinta (CCM) ameshauri kufanya matangazo kwa wananchi ya kuwazuia wasifanya kilimo hicho badala ya kusubiri wapande mazao na baadaye kuyafyeka.

“Suala la kutopanda mazao marefu ni la kisheria, lakini wapo watu ambao hawajui kama ni kosa kwa maana hiyo nashauri yafanyike matangazo kwa kila kata kama inavyofanyika kwenye siku ya usafi itakuwa shida kubwa na kuna uwezekano wa kutengeneza migogoro na wananchi pale ambapo tutasubili watu waanze kupanda mazao yao na baadaye kuyafyeka.

“Wananchi wanatakiwa kupewa elimu mapema na kila diwani afanye wajibu wake wa kutoa elimu kwa wananchi ili wasiweze kuendelea kujishughulisha na kilimo cha mazao hayo na wakati mwingine watendaji nao wafanye kazi zao ya kuzuia wananchi kulima mazao marefu na badala yake wawahamasishe wa wananchi kulima mazao ya mbogamboga na nyanya,” alisema Msinta.

Naye diwani wa kata ya Kiwanja cha Ndege, Amoss Mbalanga(CCM) amemshauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kuwachukulia hatua kali maofisa watendaji ambao wananchi ndani ya kata hizo wanaendelea na kilimo ambacho hakitakiwi kisheria.

Akichangia hoja ya mkurugenzi juu ya elimu diwani wa Diwani wa kata ya Kikombo Yona Kusaja (Chadema)amesema kuwa ni wakati wa kuboresha elimu kwa kuzingatia zaidi upelekaji walimu wa kutosha katika shule hususani shule zilizopo vijijini.

Alisema ili kuboresha elimu ni vyema kuboresha miundombinu rafiki kwa walimu ikiwa ni pamoja na kuboresha makazi yao kuwapandisha madaraja pamoja na kuwapatia stahiki mbalimbali ambazo wanazihitaji na kupeleka walimu wa kutosha katika shule hizo.

Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwanfupe akizungumza na baraza la madiwani alisema kuwa ili kuweza kuwa na baraza imara ni lazima kuwa na baraza lenye umoja na mshikamano katika masuala mazima ya kimaendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!