February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Takukuru watakiwa kutoa ruhusa Sethi kuhojiwa

Wahusika wa sakata la Tegeta Escrow, kulia ni Mkurugenzi wa VIP Engineering, James Rugemalira na Mwenyekiti Mtendaji wa IPTL, Harbinder Sing Sethi

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeombwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuamuru mtuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi, Harbinder Sethi kuchukuliwa gerezani kwa ajili ya kuhojiwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Sethi na James Rugemarila wanasota rumande kutokana na kukabiliwa na mashtaka 12 ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi kwa kula njama, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi, kujihusisha na mtandao wa uhalifu pamoja na kuisababishia serikali hasara.

Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swali ametoa ombi hilo leo tarehe 25 Oktoba 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, akisema kuwa wachunguzi wa taasisi hiyo watamchukua Sethi gerezani ili kumhoji kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.

Baada ya ombi hilo, Hakimu Shaidi ali ihairisha kesi hiyo hadi tarehe 8 Novemba 2018 baada ya mawakili wa pande zote mbili kuafikiana kuhusu mahojiano hayo, ambapo Wakili upande wa utetezi, Dorah Mallaba aliieleza Mahakama hiyo kwamba, wakati mteja wake Sethi anachukuliwa maelezo, mawakili wake wawepo.

Tarehe 8 Novemba 2018, kesi hiyo inatarajiwa kutajwa pamoja na kuangalia iwapo uchunguzi wake utakuwa umekamilika.

error: Content is protected !!