March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Milioni 350 kuiangamiza Lesotho

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inahitaji kiasi cha Sh. 350 milioni kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mchezo ujao wa kutafuta tiketi ya kufuzu kucheza Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Lesotho unaotarajia kuchezwa 18 Novemba, 2018 katika mji wa Maseru. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harison Mwakyembe amewaomba wadau pamoja na taasisi mbalimbali kuweza kuisaidia timu hiyo ambayo inatarajia kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kambi ili kuikabili Lesotho katika mchezo huo muhimu ujao.

“Wadau tunaomba kuiunga mkono Taifa stars kwa hali na mali, mchezo unaotukabili sasa hivi ni wakufa na kupona tukifanya vizuri tiketi ya kwenda Afcon baada ya miaka 38 iko wazi, tumebaikiza hatua chache kushiriki Afcon 2019,” alisema Mwakyembe.

Aidha Waziri Mwakyembe aliongezea kuwa Wizara yake na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inashirikiana kwa karibu kuhakikisha timu inapata maandalizi mazuri kuelekea mchezo dhidi ya Lesotho huku akiwaomba wadau kuendelea kuchangia timu hiyo.

“Mchango wa Watanzania na Taasisi mbalimbali bado unahitajika kwa safari ya Taifa Stars kuweka kambi Afrika Kusini maandalizi dhidi ya Lesotho,” alisema Mwakyembe.

Stars ambayo kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L ikiwa na alama nne baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo uliomalizika na inahitaji kufanya vizuri katika mchezo ujao ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu AFCON.

error: Content is protected !!