November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kocha Yanga amvaa Makambo

Heritier Makambo

Spread the love

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera katika hali ya kushangaza ameonekana kutofurahishwa na kiwango cha mshambuliaji wake, Heritier Makambo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mchezo huo ulimazika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Zahera alisema kuwa mchezaji huyo anapaswa kujituma mazoezini na kupunguza vitu vya ‘hovyo’.

“Makambo anapaswa kupunguza vitu vya hovyo kama kulala usiku sana, kutokula vizuri na anapaswa kutumika vizuri mazoezini na kama hata viacha basi hatacheza,” alisema kocha huyo.

Hata hivyo Zahera aliongezea kuwa sababu ya timu yake kuondoka na ushindi finyu katika mchezo wa leo ni kwa kuwa wachezaji waliidhalau KMC kwa kuwa imetoka ligi daraja la kwanza basi wakafikili mchezo ungekuwa mwepesi kwa upande wao.

Bao pekee la Yanga katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo Feisal Salumu katika dakika ya 88 ya mchezo na kuipeleka timu hiyo kwenye nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 22 nyuma ya Azam FC huku ikiwa imecheza michezo nane mpaka sasa.

error: Content is protected !!