Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Maonyesho uchimbaji madini yaanza Geita, GGML yadhamini
Habari Mchanganyiko

Maonyesho uchimbaji madini yaanza Geita, GGML yadhamini

Spread the love

MAONYESHO ya tatu ya teknolojia za uchimbaji madini mkoani Geita yanayofanyika kati ya tarehe 17 hadi 27 Septemba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea). 

Mdhamini wa maonyesho hayo ni Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ambayo imetoa Sh.200 milioni ili kugharamia usawazishaji eneo, mabanda 100 pamoja na umeme wa dharura (jenereta na mafuta yake) katika kipindi chote.

Maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika viwanja vya Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji na Mauzo Nje ya Nchi (EPZA) Mjini Geita ambalo pia limejengwa na Kampuni ya GGML kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii kwa gharama za Shilingi Milioni 800.

Maonyesho haya yatakutanisha kampuni za uchimbaji madini, wachimbaji wadogo na wa kati, wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Tanzania na nchi nyingine kwa ajili ya kuonyesha teknolojia zinazotumika katika sekta ya uchimbaji madini na fursa za uwekezaji na biashara kwenye sekta hiyo.

“GGML inajivunia kudhamini maonyesho haya kwa mwaka wa tatu mfululizo. Mwaka huu tunakusudia kutoa uzoefu wetu wa matumizi ya vifaa mbalimbali vya uchimbaji kwa kampuni nyingine lakini pia kwa wachimbaji wadogo,” alisema Simon Shayo, Makamu wa Rais wa GGML

“Tunajivunia kuendeleza ushirikiano na jamii inayotuzunguka kwa kunufaisha wafanyabiashara wa ndani wanaokusudia kufanya kazi na sisi,” alisema Shayo

alisema, anatarajia kuona ndoto ya kuwa na kituo cha uwekezaji na biashara ya nje mkoani jumo inatimia na GGML inakuwa sehemu ya mafanikio hayo kupitia mpango wake wa kusaidia jamii.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!