Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Makonda: Nisameheni
Tangulizi

Makonda: Nisameheni

Paul Makonda
Spread the love

PAUL Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ameomba msamaha kwa yeyote aliyemkosea wakati akitekeleza majukumu ya ukuu wa mkoa wa Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

“Ninaamini nimetumia uwezo wangu wote, akili zangu zote hatimaye ninaamini mwendo nimeumaliza vizuri. Kama binadamu naweza kuwa na mapungufu yangu.

“Inawezekana niliwakosea, mnisamehe nilipokwenda kinyume na mapenzi yenu lakini mfahamu nilifanya kwa mapenzi mema ya kuwatumikia wana Dar es Salaam,” amesema Makonda.

Makonda ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Agosti 2020, wakati akikabidhi rasmi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa Aboubakar Kunenge, mkuu wa mkoa wa sasa.

Makabidhiano hayo yamefanyika ikiwa zimepita siku 18 tangu Rais John Magufuli atengue uteuzi wa Makonda tarehe 15 Julai 2020.

Amesema, licha ya kelele nyingi zilizopogwa na watu juu ya utendaji wake, Rais Magufuli aliziba masikio.

“Namshukuru ikiwepo uvumilivu wake, baada ya kuteuliwa unafanya kazi, mbwa mwitu wengi wanaweza kubweka lakini rais aliziba masikio hadi nilipoondoka mwenyewe,” amesema Makonda.

Kunenge ameshukuru Makonda kwa ushirikiano wake wakati alipokuwa Katibu Tawala wa mkoa huo.

“Nashukuru umeacha milango wazi kupata ushauri wako, nakushukuru sana, pamoja na yote umekua mwalimu wangu na umenirahisishia kutekeleza majukumu yangu kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,” amesema Kunenge.

Makonda amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka minne tangu Rais Magufuli alipomteua mwezi Machi 2016 katika nafasi ya ukuu wa mkoa Dar es Salaam, kabla ya nafasi hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Utenguzi ulifanyika baada ya Makonda kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM, kumpitisha kugombea ubunge kwenye Jimbo la Kigamboni katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Hata hivyo, Makonda hakufurukuta mbele ya Dk. Faustin Ndugulile aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye alitangazwa kushinda kwenye kura hizo.

Katika mchakato huo uliofanyika tarehe 20 Julai 2020, Dk. Ndugulile alipendekezwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo kugombea tena katika uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Dk. Ndugulie alipata kura 190 huku Makonda akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 122.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!