Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Asilimia 70 wakazi Dar ni wambea – Makonda
Habari za Siasa

Asilimia 70 wakazi Dar ni wambea – Makonda

Paul Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akikabidhi ofisi kwa Aboubakar Kunenge, mkuu mpya
Spread the love

PAUL Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema, asilimia 70 ya wakazi wa jiji hilo ni wambea. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ametoa kauli hiyo wakati akikabidhi ofisi kwa Aboubakar Kunenge, mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam leo tarehe 3 Agosti 2020.

“Asilimia 70 ya huu mkoa ni wambea na wanapenda umbea kuliko chochote kile, (Kunenge) usikubali kuchonganishwa, watakutafuta mkuu wa mkoa na katibu tawala kukupa maneno ya umbea kuwachonganisha,” amesema Makonda.

Akielezea madhila aliyokutana nayo wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, amesema uongozi wake uligubikwa na maneno kutoka kwa watu.

“Nilipoondolewa mke wangu Maria alisema, niliamini maneno yameisha baada ya kucha ofisi, nikamwambia maneno ndio mtaji wangu kusemwa ndio furaha yangu,” amesema Makonda.

Aboubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na waandishi wa habari

Hata hivyo, amewashukuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kutoka na uaminifu wao kwao.

“Nawashukuru watumishi wa Mkoa wa Dar es Salaam, mazingira niliyopitia kama wangekuwa si waaminifu, ningeuawa hata kwa sumu kwa vita niliyokuwa nayo ya dawa za kuelvya na kurudisha nyumba 50 za umma.

“Kuna mambo matatu sitasahau ikiongozwa na vita ya dawa za kulevya, kila mtu alipiga kelele lakini Rais John Magufuli aliendelea kuamini kazi yangu kwa manufaa ya Watanzania, tukaibuka kidedea kwenye mapambano ya vita dawa za kulevya,” amesema Makonda.

Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo tarehe 15 Julai 2020, baada ya kuchukua fomu ya kuomba kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge katika Jimbo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

1 Comment

  • Qura’n tukufu inapendekeza kiongozi achaguliwe na anaotarajia kuwaongoza kinyume chake (kuiba kura au uda ganyifu wa aina yeyote) ni kukaribisha vurugu au kuhatarisha amani, mzalendo wa kweli ni yule anaetenda haki hivyo kulitKia taifa letu amani na upendo miongoni mwa watanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!