Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lugola: Natenda atakacho JPM
Habari za SiasaTangulizi

Lugola: Natenda atakacho JPM

Kangi Lugola, Waziri wa mambo ya Ndani. Picha ndogo wakati akiapishwa
Spread the love

KANGI Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema, anafanya kile atakacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo, mara baada ya kumaliza kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na viongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard.

Kwenye mkutano huo Lugola ameipa wiki mbili kampuni hiyo (Iris Corporation Berhard) impe majibu ya kuwa lini italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au kiasi cha Dola za Marekani Mil 14 (Tsh. Bil 32).

Lugola alisisitiza kuwa, lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli.

“Tumezungumza nao na tumekubaliana nao kwamba tuwape wiki mbili ili bodi ya kampuni hiyo ikakae ifanye maamuzi ya aidha waturudishie fedha zetu au walete mtambo.

“Lakini sisi kama nchi, huu mtambo muhimu sana, bado tuna uhitaji, sisi tungependa baada ya hiyo wiki mbili wafanye maamuzi ya kutuletea mtambo,” alisema Lugola.

Pia amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika.

Lugola alitoa agizo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu na Mfanyabiashara Jack Gotham kufika ofisini kwake Agosti 3 saa 3:00 asubuhi ili kutoa maelezo yanayojitosheleza yatakayomsaidia kutoa maamuzi sahihi kuhusiana na ufisadi wa fedha zaidi ya bilioni 32 za mtambo huo ambao hadi sasa haujafika nchini.

Lugola alidai kampuni zilizolipwa kifisadi ni pamoja na Gotham International ambayo imelipwa shilingi 2,848,878,659.75, Iris Corporation Berhard ambayo imelipwa 22,919,414,169,84, Gwiholoto Impex inayodaiwa shilingi 946,406,989,00, Sykes Travel Agent 5,979,600,00, Dk Shija Paul Rimoy 27,000,000,00, Aste Insurance 1,206,619.93, na Kampuni ya BMTL 569,192,090,00.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!