February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dirisha la Ligi Kuu kufungwa leo, TFF watoa onyo

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF

Spread the love

KUELEKEA kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa angalizo kwa klabu zinazoshiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza ambazo hazija kamilisha usajiri kupitia mfumo wa TFF FIFA Connect, hazitoongezea muda wa ziada kukamilisha swala hilo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Timu za Ligi Kuu ambazo hazijakamalisha usajili kwa njia ya mtandao mpaka sasa ni African Lyon, KMC, Mwadui na Mtibwa Sugar kwa upande wa timu zinazoshiriki ligi daraja lwa kwanza ni AFC, Ashanti United, Arusha United (JKT Oljoro), Kiluvya United, Majimaji, Mashujaa, Geita Gold (Mshikamano).

Dirisha hilo la usajili kwa klabu za Ligi Kuu na ligi daraja la kwanza linatarajia kufungwa kesho 26 Julai, 2018, majira ya saa sita usiku.

error: Content is protected !!