Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu: Ama zangu, ama za Magufuli
Habari za Siasa

Lissu: Ama zangu, ama za Magufuli

Tundu Lissu, Mgombea Urais Tanzania kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

LICHA ya kinyang’anyiro cha wagombea Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020 kuwa na wagombea 15, Tundu Lissu miongoni mwa wagombea hao kupitia Chadema amesema, wanaotikisa ni yeye na John Pombe Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Bagamoyo … (endelea). 

Lissu ambaye ni Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ametoa kauli hiyo jana Alhamisi tarehe10 Septemba 2020 wakati akizungumza katika kampeni zake wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. 

Makamu huyo Mwenyekiti wa Chadema Bara alisema, katika uchaguzi huo,  itakuwa ni ama zake au za Magufuli ambaye ni Rais wa Tanzania.

“Wagombea tuko 15 nasikia, lakini ukweli ni kwamba, hii biashara hii ya urais wa mwaka huu ni ya Magufuli na Tundu Lissu, ama zake ama zangu, ama za Magufuli ama za Tundu Lissu,” alisema Lissu huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo.

Dk. John Magufuli, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM

Wagombea wengine ni; Queen Cuthbert Sendiga (ADC), Bernard Membe (ACT-Wazalendo), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini), Hashimu Rungwe (Chaumma) na Seif Maalim Seif (AAFP).

Pia wamo, John Shibuda (Ada-Tadea), Yeremia Kulwa Maganja (NCCR-Mageuzi), Philipo Fumbo (DP), Leopard Mahona (NRA), Mutamwega Magaywa (SAU), Twalib Kadege (UPDP) na Maisha Mapya Muchunguzi wa NLD.

Kampeni za uchaguzi huo zinaendelea kwa vyama kunadi ilani kwa Watanzania na zitahitimishwa tarehe 27 Oktoba 2020.

5 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!