Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kikwete aeleza walivyotoana jasho na Mkapa mwaka 1995
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Kikwete aeleza walivyotoana jasho na Mkapa mwaka 1995

Spread the love

RAIS mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza jinsi alivyomtoa jasho Hayati Benjamin William Mkapa, katika mchujo wa mgombea Urais wa Tanzania ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu wa 1995. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lupaso, Masasi … (endelea).

Kikwete ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 29 Julai 2020, wakati akielezea mahusiano yake na Mkapa, katika shughuli ya mazishi ya mwili wa kiongozi huyo mstaafu, inayofanyika kijijini kwao Lupaso, wilayani Masasi mkoani Mtwara.

Hayati Rais Mkapa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, alifariki dunia kwa mshtuko wa moyo, Alhamisi tarehe 23 Julai 2020 saa 3:30 usiku, hospitalini jijini Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu.

          Soma zaidi:-

Kikwete amesema katika mchakato wa uteuzi wa mgombea wa CCM Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa 1995, alichuana vikali na Mkapa, ambapo mara ya kwanza alimshinda.

Kiongozi huyo wa Serikali ya awamu ya nne amesema, licha ya kushinda katika mchujo wa kwanza, kura hazikutosha hali iliyosababisha mchujo huo kurudiwa mara ya pili, ambapo Hayati Rais Mkapa aliibuka mshindi.

Hata hivyo, Kikwete amesema, awali alimuahidi Mkapa kwamba angemuunga mkono katika harakati zake za kugombea Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi huo, lakini baadaye kuna kitu kilichomsukuma kujitosa kwenye mchujo huo.

“Wakati huo tunaanza mchakato wa mwaka 1995 kabla ya kusukumwa kuingia huko, nilimwambia wewe unafaa kuwa rais na mimi nitakuunga mkono, lakini baadae, nilisukumwa tukagombea wote nikashind awamu ya kwanza kura hazikutosha tukarudia akanishinda,” amesema Kikwete.

Licha ya kuchuana naye katika mchakato huo, Kikwete amesema, Mkapa hakumuacha bali alimteua kuwa waziri wake wa mambo ya nje, nafasi aliyoihudumu kwa miaka 10 mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.

“Aliposhinda, akaniteua kuwa waziri wa mambo ya nje wizara kubwa si kama wizara nyingine. Ni ndogo lakini inakupa kukubalika sana.  Nimekuwa waziri wake kwa miaka 10, katika hali ya kawaida ya siasa zetu wakati mwingine mtu umeshindana naye kwa karibu vile, ni kutoonekana kabisa karibu na wewe,” amesema Kikwete.

Kikwete amesema, Mkapa enzi za uhai wake alikuwa kiongozi mwenye moyo thabiti na hakupenda kusifiwa.

Kikwende ameanza kuzungumza akisema, “ni ngumu sana kupata maneno mazuri ya kuelezea na kumuaga kaka yangu Benjamini William Mkapa. Nimemfahamu kwa miaka mingi, mimi nikiwa mwanafunzi yeye akiwa editor, waziri.”

Amesema, nimefanya naye kazi kwa karibu nilipokuja kuwa katibu wa CCM Masasi yeye akiwa mbunge wa Nanyumbu. Alikuwa mbunge wangu, mimi nikiwa katibu wake.

“Alipokuwa akisafiri nje ya nchi, akirejea lazima aje jimboni kwake, alikuwa karibu sana na wananchi wake, alikuwa anashughulikia matatizo yao na wanampa na mengine na kuwaambia anakwenda kuyafanyia kazi na mimi alipokuja kuniteua kuwa mbunge na naibu waziri wa nishati na madini nikiwa hapa katibu,” amesema

Kikwete aliyekuwa Rais wa Tanzania kati ya mwaka 2005 hadi 2015 amesema, “kama kuna jambo hasubiri umwite, anakwambia nakuja, unamwmabia njoo, anakuja anakwambia kuna hili na lile, kwa miaka kumi yangu ya urais, nilipitia changamoto kadhaa, muda mwingine mambo yanakuwa magumu lakini Mzee Mkapa alisimama na mimi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!