Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya uvamizi: Sheikh Ponda arudishwa kortini
Habari MchanganyikoTangulizi

Kesi ya uvamizi: Sheikh Ponda arudishwa kortini

Sheikh Issa Ponda, Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
Spread the love

SHEIKH Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, leo tarehe 11 Juni 2019 anapandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Rufani, jijini Dar es Salaam baada ya serikali kumkatia rufaa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kiongozi huyo wa Kiislam, anapandishwa tena kizimbani kusikiliza rufaa katika Mahakama ya Rufaa baada ya serikali kutoridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu kumfutia hukumu ya Mahakama ya Kisutu katika kesi ya jinai namba 245 ya 2012.

Jaji Augustine Shangwa wa Mahakama Kuu, tarehe 27 Novemba 2014 alifuta hukumu iliyotolewa na Mahakaka ya Kisutu iliyomtia hatiani Sheikh Ponda, kwenye kesi yake ya uvamizi wa kiwanja cha Markaz kilichopo Chang’ombe jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo iliyokuwa ikimkabili na wenzake 49, Mahakama ya Kisutu ilimtia hatiani Sheikh Ponda kwa kosa la kuingia kijinai katika eneo la ardhi ya Kampuni ya Agritanza Ltd, eneo la Chang’ombe Markazi, eneo ambalo lilikuwa likimilikiwa na Waislam.

Pamoja na Mahakama ya Kisutu tarehe 9 Mei 2013 chini ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa kumtia hatiani Sheikh Ponda, mahakama hiyo ilimwachia huru huku ikimpa sharti la kutotenda kosa lolote katika kipindi cha miezi 12 kwa mujibu wa kifungu ncha 25 (g) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu.

Sheikh Ponda kupitia wakili wake Juma Nassoro, alikata rufaa hukumu hiyo katika Mahakama Kuu akieleza kutokubaliana nayo. Mahakama Kuu ilitengua hukumu hiyo na kumwacha Sheikh Ponda huru bila masharti yoyote.

Hata hivyo, serikali ilikata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, leo Sheikh Ponda atasimama mahakamani hapo ili kusikiliza rufaa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!