Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli: Mungu amewaumbua
Habari za Siasa

Rais Magufuli: Mungu amewaumbua

Spread the love

RAIS John Magufuli amesema, Mungu amewaumbua watu waliodhihaki hatua ya serikali kufanya mazungumzo na Kampuni ya Bharti Airtel International mwaka mmoja uliopita. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Juni 2019, Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati kampuni hiyo ikikabidhi hundi ya Sh. 3 Bilioni ikiwa ni gawio pamoja na Sh. 2.7 Bilioni kuunga mkono juhudi za serikali katika maendeleo.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Rais Magufuli amesema, wapo waliodhihaki na kucheka mazungumzo hayo yaliyochukua kipindi cha mwaka mmoja.

“Wapo waliodhihaki, waliocheka,  waliojua hiki hakiwezekani lakini ninafikiri watu wote waliotutakia mabaya Mungu amewaumbua, kwasababu mazungumzo haya yamefikia mwisho,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, mazungumzo hayo yamezaa matunda, ikiwemo kampuni ya Airtel ambayo itaigawia serikali Sh. 1 Biloni kila mwezi, katika kipindi cha miezi 60 mfululizo, fedha hizo zikikusanywa zitakuwa Sh. 60 Bilioni.

Amesema, fedha hizo zikipatikana zitasaidia kuboresha huduma za kijamii, ikiwemo uboreshaji wa huduma ya afya kwa kujenga vituo vya afya.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amewapa pole viongozi walioapishwa leo Ikulu, akiwemo Dk. Edwin Mhede, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Innocent Bashungwa, Waziri wa Viwanda na Biashara, akisema kwamba majukumu yaliyo mbele yao ni makubwa.

“Nina wapongeza lakini nawapa pole, unajua Watanzania wanahitaji matokeo, ukitaka maneno mazuri kaelezwe na mke wako au mume wako.

“Sisi tunahitaji matokeo mazuri, mimi jukumu langu ni kuteua ili kusidi kiu ya Watanzania wanayohitaji ijitokeze, na ninapokutengua usifikiri nakuchukia nakupenda tu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewataka walioapishwa kutowachekea watu akisema kwamba, ni bora wachukiwe na watu kwa ajili ya utendaji kazi wao utakao mfurahisha yeye aliyewateua.

“Usimchekee mtu, nafuu wakuchukie mimi ninaekuteua nikusimamie other wise (vinginevyo) utakwenda kunusa tu na kurudi Karagwe,” amesema Rais Magufuli.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!