Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa ‘Kasi ya JPM kukopa imezidi ya JK’
Habari za Siasa

‘Kasi ya JPM kukopa imezidi ya JK’

Rais John Magufuli akiwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
Spread the love

KIASI cha fedha kilichokopwa nje ya nchini na Rais John Magufuli kwa miaka minne, kimezidi kile cha Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kwa miaka 10 aliyokaa madarakani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 18 Februari 2020, na Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Zitto ameeleza, serikali ya Rais Kikwete katika kipindi cha miaka 10, ilikopa Dola za Marekani bilioni saba, wakati serikali ya Rais Magufuli tayari imekopa Dola za Marekani Bil 9, katika kipindi cha miaka mine pekee.

“Hii serikali inakopa sana, kila siku tunaambiwa miradi inafanyika kwa fedha za ndani, serikali inajitapa hivyo, ukiangalia rekodi ya Benki Kuu ya Deni la Taifa ni kubwa sana.

“Dola bilioni 9 mkopo kwa miaka minne. Serikali ya Kikwete kwa miaka 10 ilikopa Dola 7 bilioni. Serikali imekopa Dola bilioni 2 zaidi katika miaka minne,” amesema Zitto.

Amesema, deni hilo linaongezeka kutokana na serikali kutumia fedha hizo kujenga miradi ambayo inachelewa kurudisha fedha, hali inayochangia kuzorotesha uchumi wa nchi.

“Unapojenga reli haikupi mapato hapo hapo, ndio maana uchumi ukaporomoka, inatengeneza miradi isiyolipa mapema…., mazingira ya uchumi kurudisha iwe kama 2015, inahitaji miaka 10.”

Hata hivyo, Zitto amesema serikali ina wajibu wa kukopa, lakini ilitakiwa kuchukua hatua hiyo mapema, kuliko hivi sasa ambapo inachukua mkopo wenye riba kubwa.

“Mimi sijawapinga kukopa, isipokuwa nimewaambia tayari wameharibu uchumi.  Kuja kurudisha hali yetu itakuwa ngumu. Kwenye uchumi, unapotaka uongeze mzunguko wa fedha, lazima ufanye miradi mikubwa ama ujenzi wa barabara na reli hiyo ndio nadharia inavyotaka .

“Lakini serikali ikaenda na hiyo nadharia, ikaamua kutumia fedha za kodi za wauza nyanya kufanya hiyo miradi,” amesema Zitto.

Amesema, miradi inatafuna pesa nyingi kwa kuwa, wakandarasi na malighafi vyote vinatoka nje hivyo kusababisha gharama kuwa kubwa zaidi.

“Wamerudi kukopa mkopo wa gharama kubwa. Sababu miradi inatumia wakandarasi na malighafi kutoka nje, maana yake unatumia fedha za watu unapeleka nje, ndio maana mzunguko wa fedha umeporomoka. Ni kwa sababu ya namna serikali imeamua kutekeleza miradi yake,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!