Safu mpya ya Uongozi wa Chadema

JPM apiga kijembe Chadema

Spread the love
RAIS John Magufuli na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ‘amerusha dongo’ kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akisema, ‘kukimbia changamoto ni uoga.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tarehe 1 Mei 2020, Chadema kiliagiza wabunge wake kujiweka karantini kwa muda wa siku 14, ili kujichunguza kama wameambukizwa virusi vya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu vya Corona (Covid-19). Wabunge hao walirejea bungeni tarehe 15 Mei 2020.

Bila kutaja jina la chama hicho, Rais Magufuli katika hotuba yake ya kulifunga Bunge la 11 leo tarehe 16 Juni 2020, jijini Dodoma amesema, ‘kukimbia’ Bunge haikuwa ishara njema.

“Nafahamu wako wachache walikimbia, na sijui kama wamesharejea lakini niseme tu kwamba kukimbia halikuwa jambo sahihi, sababu matatizo au changamoto hazikimbiwi, kukimbia changamoto ni ishara ya udhaifu, lakini pia ni ishara ya woga, lakini pia ni ishara ya kutojiamini.

“Siku zote, njia sahihi ya kukabiliana na matatizo ni kuyakabili, na hii ndio sababu sisi tuliamua kakabiliana na corona huku tukimtanguliza Mungu. Kwa kufanya hivyo, tumeweza mpaka sasa hivi kutatua kwa kiasi kikubwa,” amesema.

RAIS John Magufuli na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ‘amerusha dongo’ kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akisema, ‘kukimbia changamoto ni uoga.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma ... (endelea). Tarehe 1 Mei 2020, Chadema kiliagiza wabunge wake kujiweka karantini kwa muda wa siku 14, ili kujichunguza kama wameambukizwa virusi vya Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu vya Corona (Covid-19). Wabunge hao walirejea bungeni tarehe 15 Mei 2020. Bila kutaja jina la chama hicho, Rais Magufuli katika hotuba yake ya kulifunga Bunge la 11 leo tarehe 16 Juni 2020, jijini Dodoma amesema, ‘kukimbia’ Bunge haikuwa ishara njema. “Nafahamu wako wachache…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!