RAIS John Magufuli amesema, Jimbo la Singida Mashariki limechelewa kupata maendeleo, kutokana na kutelekezwa na aliyekuwa mbunge wake, Tundu Lissu. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Septemba 2019, alipomuona Miraji Mtaturu (CCM), Mbunge wa Singida Mashariki katika hafla ya uzinduzi wa rada iliyosimikwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).
Kiongozi huyo wa nchi ameeleza kuwa, baada ya jimbo hilo kumpata Mtaturu, serikali yake itashughulikia changamoto zake hususan maji na zingine.
Ametoa ameahidi hayo kufuatia ombi la Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa serikali yake, kuhakikisha jimbo hilo linaondokana na changamoto ya uhaba wa maji.
“….Laini pia namuona mheshimiwa wa lililokuwa jimbo limetelekezwa, lilikuwa la Tundu Lissu ameshika huyu. Safi sana, hongereni, mpigieni makofu na ameingia na kazi sababu saa nyingine kwenye majimbo yanakosa uwakilishi,” amesema na kuongeza.
“Na siku ile ulitoa maagizo mheshimiwa spika kwamba, tushughulikie miradi ya maji ya kule kama tulivyoshughulikia Dar es Salaam, nakuahidi tutashughulikia maji katika jimbo lile ili yale yaliyokuwa yamechelewa, yafike harakaharaka.”
Leave a comment