April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Askofu Ruwai’chi atolewa ICU

Spread the love

MHASHAMU Yuda Thadeus Ruwai’chi, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, ametolewa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kiongozi huyo wa kiroho mepelekwa katika wodi ya kawaida, baada ya hali yake kiafya kuanza kuimarika.

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 16 Septemba 2019, na Kitengo cha Uhusiano cha Taasisi ya mifupa (MOI).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, jopo la wataalamu saba wanaomhudumia Askofu Ruwai’chi limemamua kumhamisha kutoka ICU kwenda wodi za kawaida, baada ya kujiridhisha na maendeleo ya afya yake.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba, awali jopo hilo la wataalamu lilifanya tathimini ya vipimo pamoja na taarifa mbalimbali za maendeleo ya Askofu Ruwai’chi tangu alivyopokelewa na kufanyiwa upasuaji MOI tarehe 9 Septemba 2019.

“Taasisi ya MOI inawahakikishia Watanzania wote hususan waumini wa Kanisa Katoliki kwamba Askofu Ruwai’chi yuko salama na afya yake imeimarika sana hivyo waendelee kumuombea ili arejee kwenye majukumu yake,” inaeleza taarifa hiyo.

error: Content is protected !!