IGP Simon Sirro

IGP Sirro: Magaidi 300 walivamia Mtwara

Spread the love

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema, magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoa wa Mtwara na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauji. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

“Madaigi wapatao 300 kutoka Msumbiji, walivamia Kijiji chetu cha Kitaya na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji,” amesema IGP Sirro aliyekuwa anazungumzia hali ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020.

IGP Sirro amesema, “tumefuatilia baadhi ya watu, wamekamatwa na wengine ni wa kwetu hapa tumewakamata tunaendelea kuwahoji.”

“Ukifanya uhalifu Tanzania na damu ya Mtanzania haiwezi kwenda hivi, waliofanya mauaji wengine wamerudi Msumbiji na wengine tumewakamta.”

IGP Sirro amesema, “tunaendelea kupambana nao ili kuupata mtandao wote ulioanzia kule Kibiti na Rufiji ambao tulipambana nao wakaona wameshindwa.”

Mkuu huyo wa jeshi amesema, watahakikisha wanakamatwa iwe wanakwenda Msumbiji, Kenya au kwingineko ili “mwisho wa siku haki itandendeka na watakamatwa na kupelekwa mahakamani.”

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema, magaidi zaidi ya 300 kutoka Msumbiji walivamia Kijiji cha Kitaya Mkoa wa Mtwara na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauji. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea). “Madaigi wapatao 300 kutoka Msumbiji, walivamia Kijiji chetu cha Kitaya na kufanya uhalifu mbalimbali ikiwemo mauaji,” amesema IGP Sirro aliyekuwa anazungumzia hali ya usalama kuelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28 Oktoba 2020. IGP Sirro amesema, “tumefuatilia baadhi ya watu, wamekamatwa na wengine ni wa kwetu hapa tumewakamata tunaendelea kuwahoji.” “Ukifanya uhalifu Tanzania na damu ya Mtanzania haiwezi kwenda hivi, waliofanya mauaji wengine wamerudi Msumbiji na wengine tumewakamta.” IGP Sirro…

Review Overview

User Rating: 0.75 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!