Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Magufuli ahuisha ndoto ya Mwalimu Nyerere 1978
Habari za Siasa

Magufuli ahuisha ndoto ya Mwalimu Nyerere 1978

Spread the love

KIWANDA cha kutengeneza bidhaa za ngozi, kilichoanzishwa na Mwalimu Julius Kambarahe Nyerere mwaka 1978 na kisha kuzorota, kimefufuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Kiwanda hicho kilichopo Mkoa wa Kilimanjaro, kimefunguliwa leo Alhamisi tarehe 22 Oktoba 2020 na Rais John Magufuli akisema, Mwalimu Nyerere alikianzisha ili kutengeneza viatu kwa ajili ya askari wetu.

“Historia ya kiwanda hiki ilianza mwaka 1978 ambapo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliamua kukijenga ili atengeneze viatu kwa ajili ya askari wetu waliokuwa vitani kupambana na Nduli Idd Amin kule Uganda.

“Hapo katikati kazi za kiwanda hiki ilizorota, hivyo tulipoingia madarakani tulielekeza Jeshi la Magereza kukifufua. Nashukuru sana uongozi wa Jeshi la Magereza kupitia kampuni yao ya Prison Cooperation Soul, walifanyia kazi wito na kuanza kukifufua kiwanda hiki,” amesema Rais Magufuli

“Kwa kudhihirisha ndoto ya baba wa Taifa, lakini kwa kuwapenda wananchi wa Kilimanjaro nikasema kiwanda hiki kikubwa lazima kijengwe.”

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema, kiwanda hicho kitatumia malighafi inayopatikana kwa wingi hapa nchini.

“Kinatumia malighafi inayopatikana kwa wingi ambayo ni ngozi. Tanzania inashika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya mifigo barani Afrika. Tuna ng’ombe milioni 33.4, tuna mbuzi milioni 21.3, tuna kondoo milioni 5.65, tuna punda 657387.

“Kiwanda hiki ni muhimu sana, kwa sababu kitatoa ajira nyingi zipatazo 3,000,000 lakini ajira ya hapa hapa ya vijana ambayo ni ya direct (moja kwa moja), ni ya watu 300,000,” amesema.

Amesema, takwimu zinaonesha, wastani kwa mwaka mmoja Tanzania inahitaji jozi 54,000,000 za viatu na pia zinahitajika pochi, mikoba, mikanda, majaketi ya ngozi.

“Nawapongeza sana wamiliki wa kiwanda hiki, kwanza Jeshi la Magereza ambalo linamiliki asilimia 14 ya kiwanda,” amesema.

Amesema, anajua kwamba Mkoa wa Kilimanjaro hauna mifugo mingi kama ilivyo Shinyanga na mikoa mingine, lakini kwa kuwapenda aliamua kufufuliwa kwa kiwanda hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!