Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hakimu amgeuzia kibao Lissu
Habari za Siasa

Hakimu amgeuzia kibao Lissu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

THOMAS Simba, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemtaka Tundu Lissu kufika katika mahakama hiyo tarehe 19 Desemba 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea). 

Amri hiyo imetolewa jana tarehe 21 Novemba 2019, Hakimu Simba baada ya mdhamini wake, Ibrahim Ahmed kuieleza mahakama, kuwa Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, amepona.

Mdhamini huo alieeleza mahakama, kwamba amewasiliana na Lissu ambaye alimjibu, kuwa amepona lakini hawezi kurejea nchini kwa kuhofia usalama wake.

Ni baada ya Hakimu Simba tarehe 23 Oktoba 2019, kuwataka wadhamini wa Lissu kupeleka uthibitisho wa afya ya mdhaminiwa wao ambaye yupo nchini Ubelgiji.

“Lissu amesema kwa sasa amepona, ila hawezi kuja Tanzania kuhofia usalama wake,” Ibrahim aliieleza mahakama hiyo jana.

Baada ya kauli ya Ibrahim, kwamba Lissu anahofia usalama wake kurejea nchini, Hakimu Simba alisema ‘hatutaki mambo ya siasa hapa, namtaka Lissu aje hapa mahakamani kesi yake iendelee.”

Hakimu huyo alisema, ifikapo tarehe 19 Desemba 2019, wakati kesi hiyo itatajwa, anataka kumwona Lissu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki, mbele yake.

Kwenye kesi hiyo, Lissu na wenzake watatu – Simon Mkina, mhariri wa gazeti la MAWIO,  Jabir Idrissa, mwandishi wa gazeti hilo na Ismail Mehbob, mfanyakazi wa kampuni ya uchapishaji magazeti Jamana – wanakabiliwa  na mashitaka matano mahakamani, likiwamo uchochezi.

Wote wanne, wanatuhumiwa kuandika, kuchapisha na kusambaza taarifa hizo kwenye gazeti la MAWIO la tarehe 14 Januari 2016, kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Lissu yupo nje ya nchi akiwa amemaliza matibabu, ni baada ya kushambuliwa kwa risasi tarehe 7 Septemba 2019, akiwa nyumbani kwake eneo la ‘Area D’ jijini Dodoma na kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa huo, kisha alipelekwa Nairobi na baadaye Ubelgiji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!