October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto apigwa kalenda

Spread the love

HAKIMU Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam, Huruma Shaidi ameahirisha kesi ya uchochezi namba 327/2018, inayomkabili Zitto Kabwe kutokana na shahidi wa Jamhuri kutohudhuria. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Leo tarehe 22 Novemba 2019, Wakili wa Serikali Mwanandamizi, Nassoro Katuga na Wakili wa Mkuu Serikali, Tumaini Kweka wameieleza mahakama hiyo, kuwa shahidi wao anumwa.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, anatuhumiwa kufanya uchochezi alipozungumza na waandishi wa habari tarehe 18 Desemba 2018, makao makuu ya chama hicho Kijitonyama, jijini Dar es Salaam kuhusu mauaji yaliyotokea Uvinza, mkoani Kigoma

Hakimu Shaidi ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 3 Desemba 2019.

error: Content is protected !!