Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CUF ‘wamchomea’ Lissu, Membe
Habari za Siasa

CUF ‘wamchomea’ Lissu, Membe

Mhandisi Mohamed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma CUF (kulia)
Spread the love

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeeleza, rais hapaswi kuchaguliwa kwa kuhurumiwa kutokana na kupigwa risasi ama kufukuzwa kwenye chama chake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Na kwamba, kiongozi anayehitajika kuongoza taasisi ya urais shurti awe na maono makubwa na aliyetangulia wengine kufikiri na hivyo, mtu huyo ni Profesa Ibrahim Lipumba, mgombea urais kupitia chama hicho.

Mhandisi Mohamed Ngulangwa, Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma CUF, ametoa kauli hiyo jana tarehe 6 Agosti 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho Buguruni, jijini Dar es S alaam.

“Urais ni Taasisi, hautolewi kwa kuhurumiana. Ni jambo baya sana kumpiga mtu risasi. Anayefanya hivyo anastahili kulaaniwa na aliyefanyiwa anastahili kupewa pole na kuhurumiwa.

“Hata hivyo, hatuwezi kugawa urais kwa Mtanzania eti kwa kuwa kapigwa risasi au kafukuzwa kwenye chama chake,” amesema Mhandisi Ngulangwa na kuongeza:

“Kugawa urais kwa vigezo hivi tu ni kuinajisi Ikulu na kutojua thamani ya Taasisi ya Urais. Hawa wanastahili pole za kawaida za kibinadamu na kutembelewa ili kuwafariji.”

Licha ya kutotaja majina, kauli ya Ngulangwa inawalenga Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema), ambaye tayari ameteuliwa na chama hicho kugbea urais kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Tarehe 7 Septemba 2017, Lissu alipigwa zaidi ya risasi 15 zilizoingia kwenye mwili wake, ‘Area D’ jijini Dodoma muda mfupi baada ya kutoka kwenye shughuli za Bunge, alianza kutibia Dodoma, kisha alipelekwa Nairobi nchini Kenya na baadaye alipelekwa Ubelgiji kwa matibabu zaidi.

Bernard Membe, mwanachama mpya wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameteuliwa na chama hicho kugombea urais. Memba alijiunga na chama hicho baada ya kufutwa uanachama wake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bernard Membe

Ngulangwa amesema, Prof. Lipumba anafaa kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, kwa kuwa anaweza kuivusha katika matatizo ya kiuchumi.

“Kwa nchi yenye matatizo ya Kiuchumi na Kimaendeleo katika kila Sekta, inahitaji Rais anayeyajua kwa undani matatizo yetu na imekuwa ni kawaida yake (Prof. Lipumba ) kuwatangulia wengine katika kuwaza,” amesema Mhandisi Ngulangwa.

Mhandisi Ngulangwa ameeleza kuwa “nchi inahitaji rais mwenye kuona ambapo wenzake hawawezi kuona na akajitahidi kuwaonesha. Nchi inahitaji Rais Mkweli, asiyekuwa tayari kulipaka rangi ya dhahabu fuko la bangi.  Prof. Ibrahim Lipumba ni mchumi mbobezi mwenye rekodi za Kitaifa na Kimataifa.”

Ngulangwa amesisitiza urais ni nitaasisi nyeti, haiwezi kutolewa  kwa kuhurumiana.

1 Comment

  • Kweli CUF ni chama cha kubomoa upinzani, maana nilitegemea watajikita kuonyesha mapungufu ya chama kilicho madarakani ili wapewe dhamana ya kuendesha dola. Badala yake wanajikita kushambulia wapinzani wenzao, at least they have shown their true colors sitomlaumu tena Maalim Seif

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!