Chadema kushushia rungu wabunge waasi

Spread the love

KAMATI Kuu (CC) ya Chama cha Demecrasia na Maendeleo (Chadema), imeanza kuwajadili wabunge wake 16 walioamua kuasi maelekezo ya mwenyekiti wao, Freeman Mbowe. Anaripoti  Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Habari kutoka ndani ya chama hicho ambazo zimethibitishwa na mmoja wa viongozi wake wake wa juu zinasema, moja ya ajenda ya Kamati Kuu, ni kujadili “mwenendo wa wabunge waasi.”

Mbowe alielekeza wabunge wa Chadema, kutohudhuria vikao vya Bunge kwa maelezo kuwa ndani ya ukumbi na viwanja vya Bunge, siyo eneo salama. Alisema eneo hilo kumejaa virusi vya Corona.

Chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimepasuka, kufuatia hatua ya wabunge wake kadhaa, kuamua kukaidi maelekezo yanayowataka kutoingia bungeni kwa muda wa angalau siku 14 ili kujikiga na gonjwa hilo hatari.

Baadhi ya wabunge wakiongozwa na wabunge wakongwe na tegemeo ndani ya chama hicho,  akiwamo Willifred Lwakatare, mbunge wa Bukoba Mjini; Jafary Michael, Mbunge wa Moshi Mjini na David Silinde, mbunge wa Momba,  wamegoma kutekeleza maelekezo ya Mbowe kwa maelezo  kuwa siyo shirikishi.

Aidha, Silinde ambaye alikuwa katibu wa wabunge wa Chadema, alifika mbali zaidi, baada ya kuamua kujiulu wadhifa wake wa ukatibu; nafasi ambayo ilikuwa inamuwezesha kuingia kwenye vikao vya juu vya Sektarieti ya chama hicho na Kamati Kuu.

Wengine waliokadi maelekezo hayo, ni Mbunge wa Viti Maalum mkoani Lindi, Latifa Chade; Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali; Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu; Mbunge wa Viti Maalum,  mkoani Kigoma, Sabrina Sungura; mbunge  wa Viti Maalum Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mariam Msabaha.

David Silinde, Mbunge wa Momba (kushoto). Kulia ni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini

Katika orodha hiyo, wapo pia wabunge wa Viti Maalum mkoani Manyara, Rose Kamili Slaa na Anna Gideria; Mbunge wa Karatu, William Qumbaro; mbunge wa Viti Maalum mkoani Mwanza, Suzana Masele; imbue wa Viti Maalum moan Dodoma, Dk. Sware Semesi; na Risala Kaboyonga na Lucia Mlowe.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Lwakate ambaye amechaguliwa kuwa mmoja wa viongozi watatu wa wabunge waliorejea bungeni, alimtuhumu Mbowe kuamua jambo hilo zito, bila kuwapo makubaliano na wabunge.

Alisema, “hili jambo lilianzishwa na mnadhimu wetu, Esther Bulaya. Aliandika kwenye group la WhatsApp la wabunge, kwamba tusihudhurie vikao vya Bunge. Tukampinga na kumueleza kuwa hana mamlaka hayo.

“Baadaye Mbowe, akaingilia na kusema, ‘naona kuna sitofahamu kuhusu jambo hili. Naomba tuendelee kujadiliana,’” ameeleza Lwakatare.

Wilfred Leakatare, Mbunge wa Bukoba Mjini

Hata hivyo, Lwakatare anasema, “kabla ya mjadala haujafika tamati na ndani ya nusu saa, kilitumwa kwenye group hilo la wabunge, kilichoitwa, ‘waraka wa KUB’ ambako kulielekezwa wabunge wote wa Chadema, kutoingia bungeni.

“Tukaeleza hapo hapo, kwamba hiyo siyo sahihi. Kwamba mwenyekiti umefanya maamuzi hata kabla ya kukubaliana. Na hivyo, hatuwezi kuwasema Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yao bungeni kuwa hawana demokrasia, wakati na sisi tunafanya hayo hayo,” ameeleza.

Alisema, siyo sahihi kwa wabunge hao kukaa nje ya Bunge, hasa ikikumbukwa kuwa “hili ndio Bunge la mwisho na kwamba wao wamechaguliwa wananchi kuwakilisha bungeni.

Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu

Kupatikana kwa taarifa kuwa CC ya Chadema inatajadili mwenendo wa wabunge wake, kumekuja takribani wiki moja, tokea John Mnyika, katibu mkuu wa chama hicho, kunukuliwa akisema, chama chake, “kinafuatilia mwenendo wa wabunge wake waasi.”

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Tumaini Makene, mkuu wa idara ya mahusiano ya Chadema, ajenda dhidi ya wabunge, haikutajwa.

Badala yake, ajenda ya kuwajadili wabunge, imejificha kwenye kinachoitwa, “ajenda mbalimbali na hali ya ugonjwa wa COVID 19.” Mkutano wa CC utaongozwa na Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni (KUB).

KAMATI Kuu (CC) ya Chama cha Demecrasia na Maendeleo (Chadema), imeanza kuwajadili wabunge wake 16 walioamua kuasi maelekezo ya mwenyekiti wao, Freeman Mbowe. Anaripoti  Danson Kaijage, Dodoma … (endelea). Habari kutoka ndani ya chama hicho ambazo zimethibitishwa na mmoja wa viongozi wake wake wa juu zinasema, moja ya ajenda ya Kamati Kuu, ni kujadili “mwenendo wa wabunge waasi.” Mbowe alielekeza wabunge wa Chadema, kutohudhuria vikao vya Bunge kwa maelezo kuwa ndani ya ukumbi na viwanja vya Bunge, siyo eneo salama. Alisema eneo hilo kumejaa virusi vya Corona. Chama hicho kikuu cha upinzani nchini kimepasuka, kufuatia hatua ya wabunge wake kadhaa,…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Danson Kaijage

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!