Wednesday , 17 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe aendesha kikao cha kamati kuu kidigitali
Habari za Siasa

Mbowe aendesha kikao cha kamati kuu kidigitali

Spread the love

KAMATI Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imeanza vikao vyake leo Jumamosi tarehe 9 Mei 2020 kwa njia ya kidigitali chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa kwa umma na Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema imesema vikao hivyo vitajadili masuala mbalimbali ikiwamo janga la mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 na hali ya kisiasa.

Makene amesema maazimio kuhusu agenda hizo yatatolewa baada ya vikao kukamilika.

Amesema Chadema imeamua kufanya vikao vyake kwa njia ya mtandao ili kusaidia wahusija kujikinga dhidi ya corona.

“Kufanyika kwa mfululizo kwa vikao hivi kwa njia ya mtandao, Chadema imetekeleza kwa vitendo ushauri iliyotoa kwa serikali na bunge katika kuchukua tahadhari ya kupunguza mikusanyiko, katika kuendesha shughuli zake, ili kusaidia wahusika kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19,” amesema Makene.

Kikao hiko kinafanyika kipindi ambacho kumeahuhudi baadhi ya wabunge wake wakikaidi maagizo yakiyotoleaa tarehe 1 Mei 2020 ya kujitenga kwa siku 14 kwa kutofanya shughuli zozote za kibunge.

Maagizo hayo yaliyolewa na Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni baada ya vifo vya wabunge na wananchi aliodai vimetokana na corona hivyo kujitenga kwa siku 14 kwa kukaa majumbani mwao kunaweza kusaidia kutambua afya zao.

Hata hivyo, zaidi ua wabunge 12 walikaidi maagizo hayo na wamekuwa wakihudhuria vikao vya Bunge kama kawaida huku Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwaonya wale wote wanaoendelea kukaa nyumbani kwani watahesabiwa kama watoro.

Duru za siasa zinaonyesha huwenda miongoni mwa maadhimio ya kikao hicho cha kamati kuu ikawa na kuwachukulia hatua zaidi za kinidhamu wabunge hao waliokaidi.

Tayari wabunge hao wamekwisha kuondolewa katika kundi la wabunge la WhtasApp.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

Habari za Siasa

Nape: Wanasiasa, wanahabari, wafanyabiashara mteteeni Samia

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,...

Habari za Siasa

CAG: TAWA imegawa vibali vya uwindaji bila idhini ya waziri

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!