Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yatangaza kumuondoa Meya wa Dar
Habari za SiasaTangulizi

CCM yatangaza kumuondoa Meya wa Dar

Spread the love

MKAKATI wa kumuondoa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita (Chadema), umeshindwa kufanikiwa baada ya kukosekana 2/3 ya madiwani wanaotakiwa, hata hivyo wamemuondoa kinyemela. Anaripoti Hamisi Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa Kanuni za Halmashauri, wanatakiwa madiwani 17 kati ya 26 waliokuwa wanahitajika kuunga mkono Azimio la kumuondoa meya madarakani. Ni wajumbe 16 tu ndio waliounga mkono.

Taarifa za ndani zinaeleza, mpango wa kumng’oa Isaya ulipangwa kupitia tuhuma hizo, na baadaye Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuunda kamati ya kumchunguza.

Hatma ya Isaya ilipangwa kuwa leo tarehe 9 Januari 2020, baada ya Sipora Liana, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kuitisha kikao hicho kikilenga kupokea ripoti na kufikia uamuzi wa kumng’oa ama la!

Isaya anadaiwa kutotumia kiasi cha Sh. 5.8 bilioni, zilizotokana na mauzo ya hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), ambalo lilikuwa mali ya jiji.

Shirika la UDA, ambalo mwaka 1983 Msajili wa Hazina alitoa asilimia 51 ya hisa kwa Halmashauri ya Jiji, huku serikali kuu ikibakiwa na asilimia 49.

Anatuhumiwa kushindwa kuongoza kikao cha baraza la madiwani na kupendelea baadhi ya mameya kuingia katika kamati za fedha.

Pia anatuhumiwa kuwa na matumizi mabaya ya gari umma kwa kulisababishia kupata ajali, jambo ambalo meya amekuwa akijibu kwamba, yeye siyo dereva wa gari hilo.

Jana Isaya alitinga Mahakama ya Kisutu kuweka zuio ili kikao hicho kifanyike. Hata hivyo, mahakama hiyo ilipanga kutoa uamuzi wa maombi yake leo.

Wakati Isaya akikimbilia mahakamani, mkurugenzi Sipora alitangaza kuahirisha kikao hicho, na ilipofika usiku wa jana Isaya alieleza kupigiwa simu na kuarifiwa kuwepo kwa kikao hicho leo.

Vurugu ndani ya ukumbi

Awali, kuliibuka vurugu katika ukumbi wa Karimjee. Msingi wa vurugu hizo, imeelezwa kwamba kuna saini feki ya jina la mjumbe kwenye kikao hicho.

Boniface Jacob, Meya wa Ubungo ndiye aliyeshika bango, na kunyoosha juu kitabu cha mahudhurio huku akisema kuna saini feki.

“Usinisumbue, usiniguse, acha kunisukuma” Jacob alimwambia askari aliyemfuata kutaka kumshika wakati akipaza sauti kuwaeleza wajumbe kuhusu saini hiyo feki.

Wakati Jacob akipaza sauti, ukumbi ulikuwa unazizima kwa kelele na kutoelewana huku wajumbe wa Chadema wakionakana kupadwa na hasira.

“Angalia namba 18 saini hii, dunia ione” Jacob alitamka maneno hayo huku akinyoosha juu daftari la mahudhurio la wajumbe wote, “…na wamesaini, wamesaini forgery.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!