Rais John Magufuli (kulia) akiteta jambo na Spika wa Bunge, Job Ndugai

Bunge lazidi kuikaanga serikali ya Magufuli

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, imetoa mapendekezo 19 kwa serikali, yanayohitaji kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na serikali, ni kilio cha ucheleweshaji katika utoaji wa fedha za miradi ya maendeleo kama zilivyoidhinishwa na Bunge. Baadhi ya maeneo yaliyotajwa, ni sekta za kilimo, uvuvi na maji.

Akizungumza wakati wa akiwasisha taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mahamoud Mgimwa alisema, kitendo cha serikali cha kuchelewesha au kutopekeka kabisa fedha za maendeleo, kumesababisha matatizo makubwa kwa wananchi.

“Serikali haiwezi kuaminika mbele ya macho ya jamii, ikiwa haitatekeleza kwa vitendo ahadi yake ya kupelekaji fedha za maendeleo katika sekta muhimu kwa uhai wa wananchi wake,” ameeleza Mgimwa.

Alisema, “wala serikali haiwezi kuaminika ikiwa inatoza kodi hata kwenye bidhaa za maziwa na ikiwa haikumarisha ununuzi wa zao la korosho.”

Pamoja na mapendekezo hayo, Kamati ya Mgimwa imetaka serikali kuhakikisha kuwa fedha za bajeti ambazo zimepitishwa na Bunge zinapelekwa kunakohusika kama ilivyoahi bungeni.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, imetoa mapendekezo 19 kwa serikali, yanayohitaji kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na serikali, ni kilio cha ucheleweshaji katika utoaji wa fedha za miradi ya maendeleo kama zilivyoidhinishwa na Bunge. Baadhi ya maeneo yaliyotajwa, ni sekta za kilimo, uvuvi na maji. Akizungumza wakati wa akiwasisha taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mahamoud Mgimwa alisema, kitendo cha serikali cha kuchelewesha au kutopekeka kabisa fedha za maendeleo, kumesababisha matatizo makubwa kwa wananchi. “Serikali haiwezi kuaminika…

Review Overview

User Rating: 0.55 ( 1 votes)

About Mwandishi Wetu

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram