December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Magufuli azindua mahakama inayotembea

Spread the love

RAIS John Magufuli amezindua huduma ya mpya ya mahakama inayotembea barabarani ili kurahisisha huduma ya upatikanaji wa haki. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Dk. Magufuli amezindua huduma hiyo leo tarehe 6 Februari 2019 katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katika Ukumbi wa Malimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Huduma hiyo itatolewa kupitia gari lililonunuliwa na serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) kwa gharama ya zaidi ya Sh. 478 milioni.

Huduma hiyo itaanza kutolewa kuanzia ngazi ya Mahakama ya Mwanzo kwa kuwa, ngazi hiyo imetajwa kupokea idadi kubwa ya mashauri ulikilinganisha na mahakama nyingine.

Na kwamba, kwa mwaka jana zaidi ya mashauri 100,000 ambayo ni sawa na asilimia 64 ya mashauri yaliyofunguliwa katika mahakama zote nchini.

Pia Rais Magufuli amezindua mfumo wa kielektroniki wa kuratibu mashauri.

Akizungumzia kuhusu  mfumo huo, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Juma Ibrahim ametaja faida zake ikiwemo kuongeza mapato kupitia shughuli za mahakama, kujua shughuli za kila siku za mahakama na idadi ya mashauri yanayoendeshwa kote nchini.

error: Content is protected !!