Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge la Tanzania lashauri TRA isikusanye mapato ya utalii 
Habari za Siasa

Bunge la Tanzania lashauri TRA isikusanye mapato ya utalii 

Spread the love

KAMATI ya Bunge ya Bajeti imeishauri Serikali ya Tanzania kuacha utaratibu wa sasa wa ukusanyaji wa mapato yote yanayotokana na shughuli za utalii na mazao ya misitu uendelee kama ulivyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Jana Alhamisi tarehe 11 Juni 2020, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango akiwasilisha bajeti ya Serikali ya mwaka 2020/21 ya Sh. 34.87 trilioni alisema, katika kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa mapato yanayotokana na sekta ya utalii na mazao ya misitu, anapendekeza ufanywe na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mapato hayo yaingie katika Mfuko Mkuu wa Hazina.

Alisema, utekelezaji wa hatua hii utahusisha marekebisho katika Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, Sura 399, Sheria ya Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro, Sura 284, Hati ya Kuanzisha Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori ya mwaka 2014, na Sheria ya Hifadhi za Taifa, Sura 282 kupitia Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020) ili:

Dk. Mpango alisema lengo ni, kuipa TRA mamlaka kisheria ya kukusanya maduhuli yanayokusanywa hivi sasa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), na Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori (TAWA);

Leo Ijumaa tarehe 12 Juni 2020, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mashimba Ndani akiwasilisha maoni ya kamati hiyo bungeni amesema, hatua hii imekuja kipindi ambacho mamlaka hizo zimeathiriwa kwa kiwango kikubwa na gonjwa la COVID-19 hivyo mapato yake kushuka kwa kasi na kuna wasiwasi zingeweza kushindwa kujiendesha.

“Serikali haijaweza kufafanua nia hasa ya uamuzi huu kwasababu, mamlaka hizi zimekuwa na ufanisi mkubwa katika ukusanyaji wa mapato yake na utekelezaji wa majukumu yake na Serikali imekuwa ikikusanya kodi, mchango wa asilimia 15 na michango mingine mbalimbali,” amesema Ndaki.

 

Watalii wakiwa moja ya mbuga nchini Tanzania

Ndaki ambaye ni Mbunge wa Maswa Magharibi  amesema, Kamati ingependa kujua lengo hasa la Serikali katika uamuzi huu ni lipi ukizingatia kuna mashirika mengi ya Serikali ambayo yanatoa huduma na mapato yake hayakusanywi na TRA.

“Ili utaratibu unaopendekezwa uweze kutekelezeka, tulitakiwa kwanza kupitisha Bajeti ya TANAPA, TAWA, NCCA kwenye Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ili fedha hizo zinapokuwa zinatoka mfuko mkuu wa Serikali ziweze kupitia,” amesema

“Aidha, miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa itekelezwe na TANAPA, TAWA na NCCA fedha zake zimetengwa kupitia kifungu kipi.”

“Kamati inaishauri Serikali kuangalia upya uamuzi wake na kuhakikisha kwanza katika kipindi hiki kigumu mamlaka hizi zinatekeleza majukumu yake kikamilifu na uamuzi wa kuyachukua mapato au la ufanyike pindi hali ya sekta ya utalii itakapo tengemaa,” amesema Ndaki

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online & MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!