Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Askari waliokamatwa mauaji ya Akwilini waachiwa huru
Habari Mchanganyiko

Askari waliokamatwa mauaji ya Akwilini waachiwa huru

Kamanda Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Spread the love

ASKARI waliokamatwa kwa ajili ya uchunguzi wa mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilini Akwilina wameachiwa huru baada ya uchunguzi kutobaini kama wamehusika na tukio hilo. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baada ya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo imebainika kuwa askari hao hawakuhusika na mauaji hayo hivyo wameachiwa huru.

Mambosasa amesema taarifa zinazoelezwa kuwa risasi ya askari huenda ndiyo zilizotumika kufanyia katika mauaji ya Akwilini na kwamba wafuasi wa Chadema waliokuwa wakiandamana hawakuwa na siraha ni habari za hisia tu na siyo shemu ya uchunguzi uliofanywa.

Katika hatua nyingine Kamanda Mambosasa amewataka watu kutorudisha pesa walizotumiwa kwa kudaiwa kukosewa katika miamala ya simu zao za mkononi, wakitakiwa kufanya hivyo na watu wasiowafahamu.

Mambosasa ametoa agizo hilo huku kukiwa na wimbo la wizi wa pesa kwa njia ya mtandao ambapo njia mbalimbali hutumika katika kutekeleza wizi huo.

“Kama itatokea mtu amekutumia pesa kimakosa ipo kwenye akaunti yake wewe mtake aende kwenye mtandao husika wahudumu wa Vodacom wao wana uwezo wa kuzuia na baadaye wanaihamisha kutoka kwenye akaunti yake kwenda kwenye akaunti yako, wajiepushe watu kurudisha hela kienyeji,” amesema Mambosasa.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!