Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Polisi waua jambazi Mwanza
Habari Mchanganyiko

Polisi waua jambazi Mwanza

Spread the love

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Seleman Israel ‘Akayesu’ (54) anayetuhumiwa kuwa jambazi amefariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu kuwatoroka askari polisi wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 24, 2018 kwa vyombo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed Msangi .

Akielezea tukio hilo, DCP Msangi amesema lilitokea alfajiri ya leo kwenye maeneo ya Luchelele wilayani Nyamagana, ambapo marehemu Akayesu pamoja na mwenzake anayefahamika kwa jina la Salivatory Emmanuel ‘Katiyari’ walikamatwa na polisi kwa tuhuma za kujihusisha na ujambazi wa kutumia silaha.

DCP Msangi amesema majambazi hao baada ya kufanyiwa mahojiano walikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ikiwemo tukio la mauaji ya mlinzi aliyekuwa lindoni maeneo ya Igombe mkoani humo.

“Baada ya majambazi hao kukamatwa walifanyiwa mahojiano na polisi na kukiri kuwa na silaha wanayotumia katika uhalifu na wameificha maeneo ya Luchelele, askari waliongozana na whaalifu hao hadi eneo hilo na baada ya kuitoa walikurupuka na kuanza kukimbia,” amesema.

Kamanda Msangi ametoa onyo kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza hasa vijana kuacha tabia ya kujihusisha na uhalifu na kuwaomba raia wema kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ililiweze kudhibiti uhalifu mkoani humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

Habari Mchanganyiko

Kairuki awaweka mtegoni wakurugenzi watakaoshindwa kufikia malengo ya makusanyo

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na...

error: Content is protected !!